Wednesday, April 24, 2024

WAHANGA WA MAFURIKO KYELA WASHUKURU KWA MSAADA WA CHAKULA

Waathirika wa mafuriko kata ya mwaya Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya wamemshukuru Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson kwa mchango wa mahitaji mbalimbali ya chakula.

Wakitoa shukrani hizo leo Aprili 24, 2024 kwa nyakati tofauti mara baada ya Taasisi ya Tulia Trust, ikiwakilishwa na Ofisa Habari na Mawasiliano Joshua Mwakanolo kukabidhi misaada hiyo kwa niaba ya Dkt. Tulia ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya mjini.

Miongoni mwa mahitaji pamoja na mchele Kg 300, maharage Kg 50, sukari Kg 75 pamoja na unga wa ugali Kg 125.

Mwakanolo amesema kuwa baada ya kupata taarifa ya maafa hayo kupitia kwa Mbunge wa Jimbo la Kyela Ally Mlaghila waliwasilina na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU), Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson ambaye alitoa maelekezo wakawaone waathirika hao wa mafuriko.

"Tumefika hapa kwa niaba ya Dkt. Tulia angekuja mwenyewe lakini kwa sababu ya majukumu mengine ya kitaifa na kidunia tumekuja kumwakilisha kwani waanga hawa wengine ni wateja wetu kwenye Taasisi ya Tulia Trust" amesema Mwakanolo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Josephine Manase amemshukuru Dkt. Tulia na Rais Samia Suluhu Hassan kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyojitokeza .

"Namshukuru sana Rais Samia Suluhu baada ya kupata taarifa tulipokea Sh 35 milioni kwa ajili ya kusaidia mahitaji waathirika wa mafuriko pia Taasisi ya Tulia Trust chini ya Dkt. Tulia kuja kusaidia wananchi waliokubwa na janga hili" amesema Manase.

Kwa upande wake, Kaimu Ofisa kilimo, mifugo na uvuvi, Pandaleo Mushi amesema kufuatia athari hiyo ya mafuriko zaisi ya Hekta 528.3 imeathirika na itasababisha upungufu wa chakula.

Naye Mwathirika wa mafuriko, Jesca Mwakalinga amesema hali ni mbaya wanaomba serikali iwaangalie kwani changamoto ni mahitaji mbalimbali ya chakula.

"Tunamshukuru Dkt. Tulia Ackson kwa msaada mkubwa wa chakula Mungu ambariki sana" amesema Mwakalinga.

No comments:

Post a Comment