Halmashauri ya Jiji la Mbeya limepata hati safi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/24.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Dourmohamed Issa amesema leo, Jumanne Aprili 30,2024 wakati akifungua kikao cha baraza la madiwani cha kujadili taarifa za miradi ya maendeleo ikiwepo elimu na afya.
Issa amesema mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano mkubwa baina ya halmashauri, Madiwani na Mbunge wa Jimbo la Mbeya na Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson.
Issa ametaja miongoni mwa miradi iliyotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa jengo la upasuaji, wodi za wagonjwa wa upasuaji, jengo la dharula katika hosptali ya Wilaya ya Igawilo ambayo ilipandishwa hadhi baada ya kuwa kituo cha afya.

Issa amesema pia kuna ujenzi wa vituo vya afya na zahanati vinaendelea katika kata zote za Jiji la Mbeya lengo ni kuboresha huduma kwa watanzania ifikapo 2025.
Ameongeza kuwa wanaendelea kuboresha miundombinu ya elimu kama ujenzi wa matundu ya 300 katika shule za msingi na sekondari.
Sambamba na hilo amesema wamepokea gari la wagonjwa kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambalo litakadhiwa kituo cha afya Nzovwe jijini hapa ili kuboresha sekta ya afya na wananchi kujivunia matunda ya serikali yao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Jiji la Mbeya, John Nchimbi amesema kuwa wametenga zaidi ya Sh 1.5 bilioni kwa ajili ya kuboresha vyumba chakavu vya madarasa 300 kwenye shule za msingi.
Aidha amesema katika kitekekeza na kufikia malengo ya kukamilisha miradi ambayo inaelekezwa na Serikali na vyema madiwani kwenye maeneo husika kusimamia.
"Ni imani yangu kwa sasa wataalam wamekuwa wakiwashikisha kwenye miradi inayokuja katika maeneo yenu na ndio maana imetekelezwa kwa wakati uliopangwa" amesema.
No comments:
Post a Comment