Wednesday, April 3, 2024

TULIA TRUST YATOA MSAAADA WA CHAKULA, MAVAZI KWA WAZEE WASIOJIWEZA

Wazee wasiojiweza Jijini Mbeya wameanza kutabasamu baada ya  Taasisi ya Tulia Trust kuanza program  ya kugawa chakula na mavazi  bure.

Programu hiyo imeanza leo katika baadhi ya Kata lengo ni kuhakikisha wahitaji wanafikiwa huku kikosi kazi cha Taasisi ya Tulia Trust kikiendesha zoezi hilo kulingana na idadi ya waliobainika.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi hiyo, Joshua Mwakanolo amesema lengo ni kuhakikisha wazee wasiojiweza wanatabasamu kwa kupata mahitaji muhimu.

“Mpango huu ni kutekeleza  maono ya Mkurugenzi wetu ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge, na Mbunge wa Jimbo la Mbeya, Dkt. Tulia Ackson” amesema.

Amesema bado wanaenda kuhakikisha jamii inatabasamu ikiwepo ujenzi wa makazi bora  kutoa viti mwendo  kwa watu wenye walemavu.

Mkazi wa Jijini Mbeya, Lazaro Juma ameishukuru Taasisi hiyo akiwepo Mkurugenzi wake Dkt. Tulia Ackson kwa kugusa wazee waliosahaulika katika jamii na kuonekana ni wasumbufu.

“Ni mtu wa kipekee sana kwa kipindi kifupi amegusa jamii ya wenye mahitaji wakiwepo watoto wenye mazingira magumu kupata sare za shule, madaftari na hata ujenzi wa makazi bora kwa wahitaji jambo ambalo lina thawabu kubwa mbele za Mungu” amesema.

No comments:

Post a Comment