Sunday, April 7, 2024

DKT. TULIA KUMSAIDIA MATIBABU MZEE MWENYE TATIZO LA KIDONDA MGUUNI

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ametoa ahadi ya kumpatia matibabu ya mguu Mzee mwenye mahitaji  Mbaliki Shikunzi(80).

Shikunzi ambaye ni Mkazi wa mtaa Isengo Kata ya Iziwa Jijini hapa ambaye amekuwa na changamoto ya tatizo la kidonda mguu na kuishi katika mazingira magumu na kukosa msaada ikiwepo chakula, makazi hararishi.

Akizungumza kwa niaba ya Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini, Ofisa Habari na Mawasiliano Joshua Mwakanolo amesema Dkt. Tulia amehaidi kumsaidia mhitaji huyo matibabu katika Hosptali ya Rufaa Kanda sambamba na kumjengea nyumba.

Mwakanolo ametoaa kauli hiyo jana Jumapili Aprili 7 mwaka huu wakati ajitosa msaada wa mahitaji ikiwepo mchele, unga,sukari na sababu.

“Tumekabidhi  msaada wa chakula mchele kilo 20, unga wa ugali kilo 20, maharage kilo 10, sukari mifuko 3, sabuni miche 2, mafuta ya kupakaa sambamba na mavazi” amesema.

Shikungu anaishi kwenye mazingira magumu yanayopelekea kukosa mahitaji hayo muhimu na kuishi kwenye nyumba chakavu ambayo inaweza kuhatarisha maisha yake.

Mkurugenzi wake, Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini DkT. Tulia Ackson imeahidi kumjengea nyumba ya kuishi pamoja na  matibabu ya kidonda alichonacho mguuni katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.

Kwa upande wake mhitaji huyo ameshukuru Taasisi ya Tulia Trust kwa mahitaji ikiwepo ahadi ya kumpatia matibabu na kumjengea makazi bora.

No comments:

Post a Comment