Friday, April 12, 2024

MJANE AANGUA KILIO BAADA YA KUKABIDHIWA NYUMBA NA MILIONI 3.6

Mjane mwenye watoto sita Singwava Jackson (50) ameshindwa kujizuia na kuangua kilio baada ya Spika wa Bunge na Mbunge wa mjini Dkt. Tulia Ackson kumkabidhi nyumba iliyojengwa na Taasisi ya Tulia Trust ikiwa ni sadaka ya Eid El Fitri.

Singwava ambaye alikuwa akiishi kwenye nyumba iliyojengwa kwa miti na maturubahi kwa kipindi cha miaka zaidi ya mitatu baada ya kufiwa na mume akiwa anaishi Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe.

Alianza kuokota makopo baada kufukuzwa na ndugu wa marehemu mume wake akiwa na familia ya watoto sita jambo lililomlazimu kuja mkoani Mbeya kutafuta maisha huku akifanya jitihada za kuokota makopo na kuuza ili kujipatia kipato.


“Nilifukuzwa na ndugu wa mume wangu nimepitia vipindi vigumu sana, kwa kuokota makopo na kuuza kwa kilo moja Sh. 150 na kisha kufanya nahitaji ya chakula na kusomesha watoto na kujibana mpaka nikanunua kiwacha cha Sh. milioni moja huku tukilala sehemu isiyo salama” alisema Singwava.

Amesema hali yake ya kiuchumi sio nzuri licha ya kupambana kuona hapati fedheha mbele ya macho ya watu, lakini kikubwa anamshukuru Mungu kwa kiongozi huyo kuniona na kunijengea nyumba.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa,(NEC) Mkoa wa Mbeya, Ndele Mwaselela amewataka wanaCCM kusafisha njia ili ifikapo 2025 apate ushindi wa kishindo.

“Siwezi kuwa mfuasi wa shetani popote viongozi wa chama mkisimama elezeeni mambo yanayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson” amesema Mwaselela.

Mwaselela amesema CCM itaendelea kumlinda Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Spika wa Bunge Mbunge Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson na huku akiweka  bayana misaada anayotoa kwa jamii ni fedha zake sio za mfuko wa Jimbo.

Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano, Sheikh Ibrahim Bombo amesema anayoyanya Dkt. Tulia ni sadaka mbele za Mwenyekiti Mungu.

Akizungumza na maelfu ya watu waliofika katika hafla hiyo, Dkt. Tulia Ackson ameitaka jamii kujitokeza kusaidia wahitaji na kuachana na maneno.

Amesema kuwa wapo wanaozungumza pembezoni kuwa wataona mengi wajihusishamisaada hii na kampeni na kuwataka kama nao wanaweza wajitoze kusaidia wahitaji.

Dkt. amewatumia salamu na wanaomsema kwa kuwataka kuheshimiana yeye ataendelea kusaidia wahitaji kadri watakavyokuwa na uhitaji wanao mchukia watafute namna ya kusaidia na sio kupiga midomo.

No comments:

Post a Comment