Thursday, April 25, 2024

MASACHE ASHAURI MAGARI YA SERIKALI KUTUMIA MIFUMO YA GESI

Mbunge wa Jimbo la Lupa, Mkoa wa Mbeya, Masache Kasaka ameishauri serikali kuangalia uwezekano wa magari yanayoagizwa kuwa na mifumo ya gesi sambamba na kupunguza gharama za nishati hiyo.

Masache amesema hayo leo Aprili 25, 2024 lwakati akichangia hoja bungeni ya wizara ya nishati na madini  na kwamba matumizi ya mifumo ya gesi kwenye magari itakuwa chachu ya kuchochea uchumi wa nchi na  mapato ya serikali.

Amesema kwa sasa kumekuwa na mwamko mkubwa wa matumizi ya nishati ya gesi kwenye vyombo vya moto ni vyema vikaongezwa vituo mikoa mbalimbali vya usambazaji katika mikoa mingine kama Mbeya, Dodoma na kwengineko na si Dar es Salaam pekee.


 Wakati huo huo amesema wakati serikali imefanya kazi kubwa ya kuhakikisha tatizo la umeme limekwisha kikubwa iongeze nguvu katika usafirishaji na usambazaji hususan ujenzi wa kituo katika kata ya Makongorosi wilayani Chunya.

"Tumepitia kipindi kigumu cha changamoto ya umeme kwa kweli tupongeze kazi kubwa iliyofanywa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kwa kazi kubwa ya ushirikiano katika kutatua changamoto hiyo kwa watanzania” amesema Masache.

Mbunge Masache, ameomba serikali kuboresha kufikisha nishati ya umeme katika maeneo ambayo hayajafikiwa jimboni kwake katika vijiji vinavyozunguka kata ya Mafyeko, Kambikatoto na Iwalaje.

Amesema wananchi wa sasa wanahitaji umeme unawafikia wakati unakosekana kuna kuwa na malalamiko ya wananchi licha ya kuwaelekeza kuna umeme wa kutosha na ziada.

No comments:

Post a Comment