Thursday, May 9, 2024

WACHIMBAJI MADINI YA DHAHABU CHUNYA WABURUZANA MAHAKAMANI


Mashauri matatu yaliyofunguliwa Mahakama ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya kwa hati ya dharula na Aidan Msigwa dhidi ya Lucas Mbwiga Mwapenza huhusiana na mgogoro wa kitalu cha uchimbaji madini ya dhahabu eneo la Kisumaini Kijiji cha Ifumbo Kata ya lfumbo Wilaya ya Chunya yamepokelewa na Hakimu James Mhanusi kwa ajili ya kusikilizwa.

Hati hiyo imewasilishwa Mahakama ya Wilaya ya Chunya na wakili wa kujitegemea Jacqueline Massawe kwa niaba ya Aidan Msigwa wakati Lucas Mbwiga Mwapenza akitetewa na Wakili Boniface Mwabukusi akisaidiwa na wakili Irene Mwakyusa.

Mashauri yaliyowasilishwa Mahakamani na wakili Jacqueline Massawe kwa niaba ya Aidan Msigwa ni pamoja na kesi ya msingi ya kutaka kumiliki eneo lake analodai kulimiliki kihalali baada ya kulinunua, shauri la pili ni kusudio la zuio la kutofanyika kwa shughuli zozote katika eneo hilo na shauri la tatu ni kuendelea na shughuli licha ya kuwepo Kwa zuio la Mahakama.


Wakili Massawe amempatia wakili Mwabukusi hati ya dharula na nakala kuwasilishwa mahakamani na wakili Mwabukusi nae kuwasilisha pingamizi mbele ya Mahakama.

Baada ya kupokea nyaraka za pande zote mbili Hakimu James Mhanusi ameahirisha shauri hilo hadi Mei 13, 2024 Mahakama itakapoanza kuzisikiliza pande zote mbili.

Nje ya Mahakama Wakili Mwabukusi ameeleza mashauri anayedaiwa mteja wake Mahakama hapo kupitia hati ya dharula ni pamoja na  kesi ya msingi ya kutaka kulimiliki eneo lake analodai kulimiliki kihalali baada ya kulinunua pili ni kusudio la zuio la kutofanyika kwa shughuli zozote katika eneo hilo na tatu ni kuendelea na shughuli licha ya kuwepo kwa zuio la Mahakama.

Mahakama pekee ndiyo inatarajiwa kuumaliza mgogoro huo ili kuleta amani katika Kata ya Ifumbo.

No comments:

Post a Comment