Tuesday, March 19, 2024
MBEYA KUONDOKANA NA CHANGAMOTO YA MAJI MACHI 2025
Mradi huo utakaogharimu Sh 250 bilioni mpaka kukamilika ambapo katika awamu ya kwanza zitatumika Sh 119 bilioni katika hatua mbalimbali ikiwepo usanifu na ujenzi huku ukiwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni 117.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mhandisi Barnabas Konga amesema, Jana mara baada ya kutembelea eneo la utekelezaji wa mradi huo wilayani Rungwe, ikiwa ni sehemu ya kuelekea wiki ya Maji Duniani ambayo iliyoanza Machi 16 mpaka 22 mwaka huu.
Monday, March 18, 2024
WAZIRI MKUU KUFUNGUA KONGAMANO LA IDHAA ZA KISWAHILI JIJINI MBEYA
Mh. Majaliwa amewasili mkoani huo kwaajili ya kufungua Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani linalofanyika kuanzia leo March 18 - 22, 2024 katika Ukumbi wa Eden Highlands Hotel, Jijini Mbeya.
HJFMRI KUTOA MILIONI 500 KWAAJILI YA KUTEKELEZA MRADI WA DREAM, MBEYA NA SONGWE
Mwakilishi wa balozi wa Marekani nchini na Mtaalam wa masuala ya kuzuia maambukizi ya UKIMWI kutoka , WRAIR-DOD Dkt. Elick Kayange akizungumza kuhusiana na mradi wa Dreams.
Shirika la kimataifa la HJFMRI limesema linatarajia kutoa Sh 500 milioni kuwezesha mabinti balehe na wasichana vijana kupitia mradi wa dreams kwa ufadhiri wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR)
Mkurugenzi Mkuu wa HJFMRI Tanzania, Sally Chalamila amesema hayo Machi 16 mwaka huu wilayani Kyela wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa mbalimbali na mashine za kisasa vyenye thamani ya Sh 178 milioni.
Mashine na vifaa hivyo vimetolewa na Shirika la HJFMRI kupitia WRAIR-DOD kwa ufadhiri wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani (PEPFAR) kwa kushirikiana na Asasi ya Tumaini.
MWENYEKITI BAVICHA AJITOSA KUGOMBEA NAFASI YA UKATIBU MKOA WA SONGWE
Silungwe amechukua fomu kuwania nafasi Ijumaa Machi 15, 2024 na kukabidhiwa na Paul Joseph kwa niaba ya Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Gwamaka Mbughi.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu kwa mgombea, Mbughi amewataka wanachama kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama.
Tuesday, March 12, 2024
WANAFUNZI 3,000 WAPEWA MADAFTARI BURE JIJINI MBEYA
Msaada huo utagusa shule 70 katika Kata 36 za Jiji la Mbeya sambamba na kutoka viti mwendo kwa watu wenye ulamavu zaidi ya 36 ikiwa ni maelekezo ya Mkurugenzi wa Taasisi hiyo kuwagusa wahitaji.
.jpg)
Ofisa elimu msingi Kata ya Uyole akizungumza mara baada ya kupokea madaftari.
“Kupitia maelekezo ya Mkurugenzi wa Taasisi Dkt. Tulia ni kugusa walengwa shule za msingi 70 ambapo zaidi ya madaftari 600,000 yaliyotolewa kwa wanafunzi 3,000 huku idadi yake italingana na darasa analosoma mlengwa” amesema.
TULIA TRUST KUGUSA WALEMAVU KUPITIA MPANGO WA UWEZESHAJI KIUCHUMI
Taasisi ya Tulia Trust imeanza programu maalum ugawaji wa baiskeli za viti mwendo kwa walemavu sambamba na kuwaingiza kwenye mpango wa kuwezesha kiuchumi.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kubaini kundi kubwa la walemavu kuishi maisha ya tabu kwa kukosa usaidizi ikiwepo miradi ya kujipatia kipato cha kujikimu.
.jpg)
Ofisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust, Joshua Mwakanolo amesema leo Jumanne Machi 12, 2024 wakati akikabidhi kitimwendo kwa mlemavu Zaina Mbwalo (50) mkazi wa mtaa wa Kabwina Kata ya Sinde jijini hapa.
“Kupitia Mlemavu Zainabu tumebaini kuna mahitaji makubwa watakatiwa mitaji ili kuanzisha miradi ya kiuchumi".
Monday, March 11, 2024
TAASISI YA TULIA TRUST YAMKABIDHI KITIMWENDO MLEMAVU ALIBEBWA MGONGONI MIAKA SABA
.jpg)
Taasisi ya Tulia Trust leo imefanya matukio mawili likiwepo la kukabidhiwa madaftari kwa watoto wenye mahitaji maalum 3,000 katika shule la za msingi kata 36 jijini hapa.
Mbali na msaada huo pia imemgusa Mwanafunzi mlemavu wa miguu Doreen Myuki (12) anayesoma darasa la saba katika shule ya Msingi Mwasote Jijini hapa aliyekuwa akibebwa kwa miaka saba mgongoni akipelekwa shule na kurudi.
Akikabidhi msaada wa kitimwindo, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust, Joshua Mwakanolo amesema kuwa bado wataendelea kutoa viti mwendo kwa walemavu wenye uhitaji katika kata zote 36 za Jiji la Mbeya.
TECNO YAPONGEZWA KWA KUBORESHA HUDUMA YA MAWASILIANO MBEYA
Hayo yamesemwa na Afisa Michezo Mkoa wa Mbeya Robert Mfugale akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera wakati wa uzinduzi wa duka la TECNO lililopo Soweto Jijini Mbeya.
"Niwapongeze TECNO kwa kuwa wabunifu na kuona umuhimu wa kuwekeza katika mkoa wetu wa Mbeya na kuweka duka kubwa ambalo litaleta mageuzi makubwa na teknolojia, hakuna ulimwengu unaoenda bila teknolojia sasa mtu anaweza kupata taarifa kiganjani kwake" amesema Mfugale.
MASACHE AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI
Mabunge wa Jimbo la Lupa Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya, Masache Kasaka amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwepo miradi ya sekta ya Elimu ambayo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ilitoa fedha.
Katika ziara yake Masache ametembelea Kata ya Itewe sambamba na ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Chunya mjini.
Masache amesema kuwa katika mradi wa shule ya msingi Chunya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya Sh 90 milioni.
“Nina kila sababu ya kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwani imetuletea fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika miundombinu ya barabara,maji na miundombinu ya elimu” amesema.
Pia Masache alichangia mifuko 40 ya saruji kwaajili ya ujenzi wa madarasa 4 vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi.
Friday, March 8, 2024
UMOJA WA WANAWAKE MZRH WAKABIDHI HUNDI YA MIL. 37.5 KWAAJILI YA UNUNUZI WA KITANDA CHA KISASA CHA UPASUAJI WA MIFUPA
Ikiwa
ni kiliele cha Madhimisho ya Siku ya Wanamke Duniani ambayo
huadhimishwa machi 8 kila mwaka, Umoja wa Wanawake Hospitali ya Rufaa ya
Kanda Mbeya leo Machi 08, 2024 wamekabidhi hundi yenye thamani ya
shilingi Mil 37.5 kwaajili ya ununuzi wa kitanda cha kisasa kwaajili ya
Upasuaji wa mifupa hospitalini hapo.
Akipokea hundi hiyo ya Mil 37.5 Dkt. Godlove Mbwanji ,Mkurugenzi Mtendaji wa Hospotali ya Rufaa ya Kanda Mbeya ameushukuru na kuupongeza Umoja wa Wanawake Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kuwa chachu na mchango mkubwa katika maendeleo ya Hospitali na mkoa kwa ujumla.
“...ninyi mmekuwa ni chachu kubwa
sana kwa mafanikio ya hospitali na mkoa kwa ujumla nichukue nafasi hii
pia kuwapongeza wanawake wote Tanzania nzima kwa mchango mkubwa sana wa
maenedeleo ya nchi yetu.” Dkt. Godlove mbwanji
MTANDAO WA POLISI WANAWAKE WAWA KIVUTIO MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Mbeya (TPF Net) ukiongozwa na Mwenyekiti wake Mrakibu wa Polisi (SP) Kaneng Muro umepamba kilele cha maadhimisho ya siku ya mwanamke dunia ambayo kimkoa yamefanyika Ubaruku, Wilaya ya Mbarali.
Pia,
mtandao wa Polisi wanawake mkoani hapa kwa kushirikiana na Dawati la
Jinsia na Watoto umekuwa kivutio kwa washiriki wa maadhimisho hayo
ambapo elimu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi
ya watoto na wanawake ilitolewa.
Sambamba na hilo, kikosi cha usalama barabarani kilipata nafasi ya kueleza matumizi ya kidigitali ya ukusanyaji wa madeni ya makosa ya usalama barabarani, vipimo vya ulevi kwa madereva na ukamataji wa makosa ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani kwa kutumia "POS Machine".
Mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mwanamke dunia kwa Mkoa wa Mbeya alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwila kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera huku maadhimisho yamebeba kauli mbiu "Wekeza kwa Wanawake, Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii".
Wednesday, March 6, 2024
WAZEE MBEYA WAFURAHISHWA NA HUDUMA ZA AFYA
Akizungumza baada ya ziara hiyo, mmoja wa wazee alisema wamefurahishwa na maendeleo waliyoona na wanatambua juhudi zinazofanywa na wafanyakazi wa afya katika kutoa huduma bora kwa wananchi. Hata hivyo, wazee hao wametoa wito kwa serikali na wadau kuhakikisha hospitali hiyo inapata fedha za kutosha ili kuendeleza maendeleo hayo.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imepokea sifa nyingi kutoka kwa wazee hao na imewasisitizia wananchi kuchukua tahadhari na kutembelea vituo vya afya mara kwa mara kwa ajili ya ukaguzi wa afya zao. Wazee hao pia wameahidi kuendelea kushirikiana na uongozi wa hospitali ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa wazee hao, hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya inaendelea kufanya maendeleo makubwa katika utoaji huduma za afya na wana matumaini makubwa kwa mustakabali wa sekta ya afya mkoani humo.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)

.jpg)
.jpg)