Akizungumza na waandishi wa habari Machi 04, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Benjamin Kuzaga katika hafla fupi ya mapokezi ya magari na Pikipiki ameishukuru Kamati ya Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya kwa msaada wa magari na pikipiki hizo kwani zitasaidia sana katika kufanikisha kutekeleza majukumu kwa ufanisi na haraka.
Tuesday, March 5, 2024
KAMATI YA USALAMA BARABARANI YAKABIDHI MAGARI NA PIKIPIKI KWA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
MTANDAO WA POLISI WANAWAKE TANZANIA (TPF-NET) MBEYA WATOA MISAADA VITUO VYA YATIMA
Katika kulelea siku ya Wanawake duniani ambayo kilele ni Machi 8 mwaka huu Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF _Net) Mkoa wa Mbeya umetoa misaada mbali mbali kwa vituo viwili vya kulelea watoto yatima cha Nuru na St. Allamano .
Msaada huo umekabidhiwa jana Machi 4,2024 huku wakiomba Serikali kulegeza masharti ya mabadiliko ya sheria za bima afya kwa vituo vya kulelea watoto yatima.
Mwenyekiti wa Mtandao huo SP. Kanen Muro amesema kuwa sheria hiyo inavitaka vituo hivyo kuwa na watoto wasio chini ya 100 ndipo wakatiwe bima ya Sh 59,400..jpg)
“Tuombe Serikali ilione hilo ili watoto waweze kupata huduma bora za afya kwani kwenye kituo cha Nuru kina mahitaji makubwa sana na hakijafikia watoto 100 waliopo ni 33 wakiwepo walemavu” amesema.
Sunday, March 3, 2024
HOSPITALI ZA RUFAA ZA MIKOA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA ZA MASIKIO, PUA NA KOO
Wasimamizi hospatali za Rufaa za Mikoa nchini wameagizwa kuhakikisha uwepo wa vifaa ambavyo vitatumika kutoa matibabu ya masikio, koo na pua ili kufanikisha utolewaji wa huduma bora kwa wananchi.
Agizo hilo limetolewa leo Machi 03, 2024 na Mgeni rasmi Dkt. Maisara Karume wakati akihutubia kwaniaba ya Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu katika maadhimisho ya siku ya usikivu duniani yaliyofanyika kitaifa Mkoani Mbeya katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.
"Ili
kufanikisha utolewaji endelevu wa huduma hizi kwa wananchi wote,
nawaagiza wasimamizi wa hospitali zote za rufaa kuhakikisha uwepo wa
vifaa ambavyo vitatumika kutoa matibabu ya masikio, koo na pua. Vivyo
hivyo Waganga Wakuu na Halmashauri kusimamia vituo vyote vya huduma za
afya ya msingi vilivyo katika maeneo yao kwa kuweka bajeti za vituo vyao
fedha na kununua vifaa kwaajili ya kuwezesha kufanya uchunguzi wa sikio
la nje, mfereji wa sikio na ngoma ya sikio" amesema Dkt. Karume.
Pia ameongeza kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau watahakikisha watumishi wa afya wanapewa mafunzo maalum ya namna ya kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo ya usikivu, kufanya tafiti mbalimbali zinazosaidia kuboresha huduma za kuzuia na kuthibiti magonjwa yanayosababisha kupotea kwa usikivu kwa watu wazima na watoto.
Friday, March 1, 2024
PUMZIKA KWA AMANI MZEE MWINYI
Pumzika kwa Amani Rais Mstaafu wa awamu ya pili Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi.
ASILIMIA 94 WALIOTUMIA ARVs KWA USAHIHI WAMEFUBAZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KATIKA VITUO VYA AFYA 21 VYA JESHI
Watu 23,300 Tanzania Bara na Visiwani wamefanikiwa kufikia hatua ya kufubaza maambukizi ya VVU baada ya kuzingatia matumizi usahihi Dawa za ARVs.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkurugenzi wa Shirika la HJFMRI Tanzania, Sally Chalamila amesema baada ya kukabidhi ukarabati wa maabara mbili katika hosptali ya Jeshi Mbeya na Zahanati ya 514 KJ iliyopo Makambako Mkoa wa Njombe..jpg)
Chalamila amesema HJFMRI inatekeleza miradi miwili ikiwepo ya Nyanda za Juu Kusini na Jeshi, ambapo upande wa mradi wa Jeshi unatekelezwa katika vituo vya afya 21 Tanzania bara na Visiwani.
Chalamila amesema matumizi ya sahihi ya ARVs imeleta matokeo mazuri kwa wavvu 23,300 sawa na asilimia 94 kufubaza maambukizi na kubakiwa na moja ili kufikia 95.
Thursday, February 29, 2024
WAKULIMA WA TUMBAKU WATAKA ZOEZI LA UGAWAJI WA PEMBEJEO LISIMAMIWE NA CHUTCU
Vyama vya Ushirika vya Wakulima wa tumbaku Wilaya ya Chunya na Songwe wamekerwa na Muungano wa Vyama Vikuu vya Ushirika Tanzania (TCJE) kuchelewesha pembejeo za kilimo na kutaka usambazaji ufanywe na Chama Kikuu cha Wakulima wa Tumbaku (CHUTCU) ili kunusuru uzalishaji.
Kauli hiyo imetolewa jana February 29, 2024 kwenye Mkutano mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (CHUTCU) ambapo wamedai TCJE kutowafikishia mbolea kwa wakati wakuwa chanzo cha kusababisha mazao yao yasifanye vizuri shambani.
Meneja Mkuu wa Chama cha kikuu cha wakulima wa Tumbaku (Chutcu)Wilaya ya Chunya Christian Msingwa (kulia)akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mbaraka Batenga.
Mkulima na Mwanachama wa CHUTCU, mawazo mamboleo amesema changamoto ya TCJE kuchelewesha pembejeo zimekuwa zilizoathiri kwenye uzalishaji wa tumbaku na hawakubaliani na TCJE kuendelea kusambaza pembejeo za kilimo badala yake chama kikuu cha ushirika CHUTCU ndio kiwe kinasimamia.
DC HANIU AZINDUA ZOEZI LA CHANJO YA MINYOO NA KICHOCHO
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Jaffar
Haniu jana Februari 28, 2024 amezindua zoezi la chanjo ya Minyoo na Kichocho
ikiwa ni sehemu ya kutokeza magonjwa yote yasiyopewa kipaumbele katika jamii. Zoezi hilo limefanyika katika shule ya Msingi Katumba Mchanganyiko kata ya
Ibighi.
Akizindua zoezi hili Haniu ameagiza wazazi wote kuwapeleka watoto katika maeneo ya kutolea huduma hii ikiwemo Hospitali, zahanati na vituo vya afya sambamba na shule zote za Msingi na Sekondari.
MICHE YA MATUNDA NA KIVULI ZAIDI YA 100 YAPANDWA SHULE YA MPAKANI WILAYANI KYELA
Akizindua klabu ya mazingira na kuendesha zoezi la upandaji miche zaidi ya mia shule ya mchepuo wa kiingereza ya Mpakani, Mkurugenzi wa LTYF Leonatha Likalango amesema watoto wakipewa elimu ya mazingira watakuwa mabalozi wazuri kwani elimu hiyo wataifikisha kwa wazazi wao nyumbani.
Shule hiyo ni mpya na haina miti ya matunda na vivuli hivyo
miti hiyo itasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo, upepo, kuwapatia matunda watoto
na kuifanya shule iwe na mandhali nzuri na ya kuvutia.
Tuesday, February 27, 2024
CCM YATOA MWELEKEO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA KUTOWABEBA WAGOMBEA
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa ( NEC) Mkoa wa Mbeya, Ndele Mwaselela akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza msimamo wake kuelekea uchaguzi mdogo wa Serikali za mitaa kutombeba mgombea yoyote na badala yake kuwataka kujipima wenyewe kama watakubalika kwa wananchi.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa (NEC) Mkoa wa Mbeya, Ndele Mwaselela amesema Jana wakati akizungumzia msimamo wa chama kuelekea uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika hivi karibuni sambamba na kuonya walioanza kupasha kutangaza nia kabla ya wakati.
“Hao walioanza kupitapita huko wanapoteza muda kwani kuna hatua za awali za michakato kuanzia ngazi za Kata, Mitaa, Wilaya na Mkoa unafanya maamuzi na sio kwamba kila atakayechukua fomu atapitishwa na chama tunahitaji kupata mgombea anayekubalika na wananchi katika eneo lake” amesema.
Mwaselela ameweka wazi kuwa mchakato wa uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa mwaka huu ni mgumu lengo ni kutaka wananchi kupata viongozi watakaokuwa chachu ya kutatua changamoto katika jamii.
“Chama hakitambeba mtu, nasisitiza hakitambeba mtu katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni, kwa sasa tunahitaji utulivu, mpaka hapo dirisha likifunguliwe wenye sifa watakaostahili na kukubalika na wananchi wachukue fomu kwa kuzingatia kanuni na utaratibu ndani ya chama” amesema.
Amesema kama chama wanaamini wananchi ndio watawapima wagombea kwenye mitaa, vijiji, kata, na Wilaya sio chama na kupiga marufuku wanaoanza kupasha kabla ya wakati huku akisisistiza wasubiri muda ufike .
Kwa upande wake Webby Mwambulukutu amesema kwa sasa chama kisitumie nguvu ya kuwabeba na badala yake wananchi wachague viongozi ambao wataendana na kasi ya Mbunge wa Mbeya mjini na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo.
Saturday, February 24, 2024
WAZEE, WALEMAVU, WENYE MAHITAJI 6,000 WAPEWA BIMA YA AFYA NA DKT. TULIA
KAMPUNI YA PCT YATOA MSAADA WA MIFUKO 30 YA SARUJI SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI
Kampuni ya Pareto PCT imetoa msaada wa mifuko 30 ya saruji kwa Shule ya Sekondari Mwakipesile, Shule mbili shikizi katika vijiji vya Iswago Ruanda.
Kati ya mifuko hiyo 30 mifuko 10 imeelezw kutumika kwa ajili ya ambayo itatumika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu na miundombinu ya vyumba vya madarasa.
Msaada huu umetolewa na Kampuni ya PCT kupitia Afisa Pareto wa Mikoa ya Mbeya na Songwe, Mussa Malubalo.
Friday, February 23, 2024
DKT. TULIA AKABIDHI NYUMBA KWA MLEMAVU WA MACHO
Thursday, February 22, 2024
RAIS WA IPU DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA MKOA WA MBEYA
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa huku pamoja na mambo mengine wamejadili kuhusu namna bora ya kuboresha Maendeleo ya Jiji la Mbeya katika sekta mbalimbali.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)

.jpg)
.jpg)

.png)









