Wakuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwila wamekutana kutatua mgogoro wa wananchi na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) ambao wamevamia kwa ujenzi wa makazi na kilimo.
Uamuzi huo ni kutokana na maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera kwa wakuu hao wa Wilaya kukutana na TFS ili busara itumike kwa kuwaondoa katika hifadhi na kuwatengea eneo lenye ukubwa wa hekari 698.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 17, 2024 ikiwa ni siku moja imepita baada ya kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa vijiji vya Ruiwa Wilaya ya Mbarali na Malamba Wilaya ya Mbeya.
Malisa amesema kutokana na uamuzi wa busara za Rais Samia Suluhu Hassan kupitia mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuona thamani ya wakazi kwa kugawa maeneo yaliyohainishwa kwa ajili ya kilimo
Ofisa misitu TFS, Isdori Chuwa amesema kuwa watu wote waliokuwa wanalima ndani ya hifadhi ni wavamizi na ilipaswa waondolewe lakini kutokana na busara za mkuu wa mkoa wa mbeya wametengewa eneo lenye hekari 698.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwila amesema kadri siku zinavyozidi kwenda idadi ya watu imekuwa ikiongezeka katika hifadhi la mlima ambapo shughuli za kibinadamu zinafanyika zinaweza kuleta athari.
Amesema tayari wataalamu wamefanya tathmini kwa kuhainisha maeneo ambayo yataruhusiwa kulimwa na maeneo mengine yatabaki chini ya hifadhi.
No comments:
Post a Comment