Wednesday, May 29, 2024

DC MALISA AHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA DAFTARI LA MPIGA KURA

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa amewataka wananchi mkoani hapa  kujitokeza kwa wingi kujiandisha kwenye  maboresho ya dafrari la kudumu la wapiga kura  msimu utakapofika.

Malisa amesema jana Mei 28, 2024 kwa nyakati tofauti alipofanya  ziara ya kusikiliza kero  za wananchi katika kata za Tembela, Mwasanga na Kalobe Jijini hapa.

Amesema tunaelekea kipindi cha uchaguzi Mkuu Oktoba 2025 na uchaguzi mdogo wa Serikali za mitaa wananchi wanapaswa kuhamasika kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika  maboresho ya daftari la wapiga kura.


"Nitumie fursa hii kuwataka wananchi mjitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye maboresho ya dafrari la mpiga kura ili kupata fursa ya kuchagua  viongozi wazuri hata nyinyi mkitaka kugombea ni uhuru wa kidemokrasia kushiriki" amesema.

Malisa ametumia fursa hiyo kuwapa salamu za Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini, Dkt Tulia Ackson na Mkuu wa Mkoa Juma Homera ambaye hivi karibuni atafanya ya kuwatembelea.

Wakati huo huo amehaidi kuchangia Sh 500,000 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Tembele lengo ni kupunguza msingamano wa wanafunzi kwenye vyumba vya madarasa sambamba na kuhamasisha jamii kuchangia.


Malisa pia ameomba wananchi kutoa ushirikiano kwa viongozi wa Serikali za mitaa na kubainisha kuwa Mkuu wa Mkoa, Juma Homera atafanya ziara ya kusikiliza kero zao.

Kaimu Mkurugenzi Jiji la Mbeya na Ofisa Elimu Jiji Dkt. Julius Lwinga amesema serikali imeanza mchakato wa maboresho ya shule kongwe ambazo ni chakavu.

Wakati huo huo wananchi wameomba Serikali kuboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingi.

No comments:

Post a Comment