Tuesday, April 30, 2024

JIJI LA MBEYA LAPATA HATI SAFI 2023/24


Halmashauri ya Jiji la Mbeya limepata hati safi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Dourmohamed Issa amesema leo, Jumanne Aprili 30,2024 wakati akifungua kikao cha baraza la madiwani cha kujadili taarifa za miradi ya maendeleo ikiwepo elimu na afya.

Issa amesema mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano mkubwa baina ya halmashauri, Madiwani na Mbunge wa Jimbo la Mbeya na Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt.  Tulia Ackson.

Issa ametaja miongoni mwa miradi iliyotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa jengo la upasuaji, wodi za wagonjwa wa upasuaji, jengo la dharula katika hosptali ya Wilaya ya Igawilo ambayo ilipandishwa hadhi baada ya kuwa kituo cha afya.

Thursday, April 25, 2024

MASACHE ASHAURI MAGARI YA SERIKALI KUTUMIA MIFUMO YA GESI

Mbunge wa Jimbo la Lupa, Mkoa wa Mbeya, Masache Kasaka ameishauri serikali kuangalia uwezekano wa magari yanayoagizwa kuwa na mifumo ya gesi sambamba na kupunguza gharama za nishati hiyo.

Masache amesema hayo leo Aprili 25, 2024 lwakati akichangia hoja bungeni ya wizara ya nishati na madini  na kwamba matumizi ya mifumo ya gesi kwenye magari itakuwa chachu ya kuchochea uchumi wa nchi na  mapato ya serikali.

Amesema kwa sasa kumekuwa na mwamko mkubwa wa matumizi ya nishati ya gesi kwenye vyombo vya moto ni vyema vikaongezwa vituo mikoa mbalimbali vya usambazaji katika mikoa mingine kama Mbeya, Dodoma na kwengineko na si Dar es Salaam pekee.

Wednesday, April 24, 2024

WAHANGA WA MAFURIKO KYELA WASHUKURU KWA MSAADA WA CHAKULA

Waathirika wa mafuriko kata ya mwaya Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya wamemshukuru Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson kwa mchango wa mahitaji mbalimbali ya chakula.

Wakitoa shukrani hizo leo Aprili 24, 2024 kwa nyakati tofauti mara baada ya Taasisi ya Tulia Trust, ikiwakilishwa na Ofisa Habari na Mawasiliano Joshua Mwakanolo kukabidhi misaada hiyo kwa niaba ya Dkt. Tulia ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya mjini.

Miongoni mwa mahitaji pamoja na mchele Kg 300, maharage Kg 50, sukari Kg 75 pamoja na unga wa ugali Kg 125.

Mwakanolo amesema kuwa baada ya kupata taarifa ya maafa hayo kupitia kwa Mbunge wa Jimbo la Kyela Ally Mlaghila waliwasilina na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU), Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson ambaye alitoa maelekezo wakawaone waathirika hao wa mafuriko.

Sunday, April 14, 2024

MLIMA KAWETELE WAMEGUKA NA TOPE KUFUNIKA MAKAZI YA WATU

Watu kadhaa wanaripotiwa kukosa makazi mkoani Mbeya kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha kumeguka kwa Mlima Kawetele na tope la mlima huo kufunika makazi ya watu leo Aprili 14, 2024.

Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Mbeya imetembelea Mlima Kawetele uliopolomoka alfajiri ya leo na kusababisha kufukiwa kwa nyumba 20, ng’ombe wanne na kuharibika kwa miundombinu ya Shule ya Mary's iliyopo Mtaa wa Gombe, Kata ya Itezi, Jiji la Mbeya.

Akizungumza baada kuwasili eneo hilo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Juma Homera amekanusha uvumi unaozagaa mtandaoni ukidai kuwa kuna maafa katika tukio hilo ambapo amesema zaidi ya hivyo vilivyotajwa hakuna madhara mengine wala maafa kama inavyoripotiwa na baadh ya watu.

Homera ameiagiza Halmashauri ya Jiji la Mbeya kufanya tathmini juu ya waathirika hasa wale waliokosa malazi wahakikishe wanapatiwa mahali pa kujihifadhi wakati huu ambao serikali inaendelea kupambana kuhakikisha hali inakuwa sawa katika maeneo hayo.

Pia amekiagiza kitengo cha Ardhi cha Halmashauri hiyo kuacha kuwapimia wananchi viwanja eneo lenye changamoto hasa ya mkondo wa maji ili kuepuka matatizo kama hayo ambayo yangeweza kuzuilika.

Tukio hilo limetokea alfajiri ya kuamkia leo kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini. Hivi karibuni mikoa ya Arusha na Lindi pia imekumbwa na mafuriko na kusababisha vifo na uharibifu wa mali na miundombinu mbalimbali.

 

Friday, April 12, 2024

MJANE AANGUA KILIO BAADA YA KUKABIDHIWA NYUMBA NA MILIONI 3.6

Mjane mwenye watoto sita Singwava Jackson (50) ameshindwa kujizuia na kuangua kilio baada ya Spika wa Bunge na Mbunge wa mjini Dkt. Tulia Ackson kumkabidhi nyumba iliyojengwa na Taasisi ya Tulia Trust ikiwa ni sadaka ya Eid El Fitri.

Singwava ambaye alikuwa akiishi kwenye nyumba iliyojengwa kwa miti na maturubahi kwa kipindi cha miaka zaidi ya mitatu baada ya kufiwa na mume akiwa anaishi Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe.

Alianza kuokota makopo baada kufukuzwa na ndugu wa marehemu mume wake akiwa na familia ya watoto sita jambo lililomlazimu kuja mkoani Mbeya kutafuta maisha huku akifanya jitihada za kuokota makopo na kuuza ili kujipatia kipato.

Tuesday, April 9, 2024

MTOTO WA SIKU 27 AFANYIWA UPASUAJI KICHWANI NA KUONDOLEWA UVIMBE WENYE KILOGRAMU 1.8

Ikiwa ni siku ya kwanza ya kambi maalumu ya Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari Bingwa wa upasuaji wa mifumo ya fahamu, ubongo na uti wa Mgongo (Neurosurgeons) TNS, jana Aprili 08, 2024 wameanza rasmi zoezi la upasuaji kwa wagonjwa 3 waliofika hospitalini hapo wakiwa na matatizo tofauti.

Katika moja ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji, madaktari Bingwa hao wamefanikiwa kumfanyia upasuaji mtoto wa siku 27 na kuondoa uvimbe wenye kilogramu 1.8 aliozaliwa nao sehemu ya nyuma ya kichwa chake upasujia uliochukua takribani saa moja kukamilika.


Mbali na upasuaji huo wataalam hao pia wamefanikiwa kuwafanyia upasuaji wagonjwa wawili mmoja akiwa ni mtoto mwenye umri miezi 9 aliyekuwa na tatizo la mgongo wazi na kufanikiwa kufunikwa eneo hilo kupitia upasuaji uliofanyika kwa muda wa saa moja, na mgonjwa mwingine ni mtu mzima mwenye umri wa miaka 39 aliyevunjika pingili ya katikati ya uti wa mgongo baada ya kupata ajali na madaktari hao waliweza kufanikisha upasuaji huo uliochukua muda masaa mawili.

Kambi hiyo ya upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu inaendelea kwa muda wa siku tano ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, ikilenga kutoa huduma hiyo kwa wananchi wa Nyanda za Juu Kusini ikiwemo mikoa ya jirani na Mbeya.

VIONGOZI MBEYA WASEMA DKT. TULIA HAFANYI SIASA ANATEKELEZA ANDIKO LA MUNGU KUGUSA WAHITAJI

Sheikh wa Mkoa wa Mkoa Mbeya, Msafiri Njalambaha amesema kitendo anachokifanya Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani na Spika wa Bunge Dkt. Tulia kuigusa jamii ni sadaka na kutekeleza maagizo ya Mungu visihusishwe na masuala ya kisiasa.

Sheikh Njalambaha amesema usiku wa jana Aprili 8 mwaka huu wakati wa waumini wa dini ya kiislam, viongozi wa Chama, Serikali na Machifu mkoani hapa walipougana kula aftari iliyoandaliwa, Dkt. Tulia Ackson kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust.

Amesema Dkt. Tulia amekuwa msaada mkubwa kwa dini ya kiislam kwani licha ya kuwafutulisha pia amekuwa akichangia ujenzi wa misikiti, jamii yenye mahitaji.

Sunday, April 7, 2024

DKT. TULIA KUMSAIDIA MATIBABU MZEE MWENYE TATIZO LA KIDONDA MGUUNI

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ametoa ahadi ya kumpatia matibabu ya mguu Mzee mwenye mahitaji  Mbaliki Shikunzi(80).

Shikunzi ambaye ni Mkazi wa mtaa Isengo Kata ya Iziwa Jijini hapa ambaye amekuwa na changamoto ya tatizo la kidonda mguu na kuishi katika mazingira magumu na kukosa msaada ikiwepo chakula, makazi hararishi.

Akizungumza kwa niaba ya Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini, Ofisa Habari na Mawasiliano Joshua Mwakanolo amesema Dkt. Tulia amehaidi kumsaidia mhitaji huyo matibabu katika Hosptali ya Rufaa Kanda sambamba na kumjengea nyumba.

Thursday, April 4, 2024

TULIA TRUST YAKABIDHI KILO 400 ZA MCHELE MSIKITI MKUU WA MKOA WA MBEYA

Taasisi ya Tulia Trust imetoka kilo 400 za mchele na tende boksi 20 katika Msikiti Mkuu wa Mkoa wa  Mbeya kwa ajili ya waumini wenye mahitaji katika kuelekea sikuu ya Eid El Fitri.

Ofisa habari na mawasilino wa Taasisi ya Tulia Trust Joshua Mwakanolo amekabidhi mahitaji hayo kwa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Msafiri Njalambaha katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya msikiti wa Mkoa barabara ya Saba jijini hapa.

Akizungumza kwa niaba ya Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson, Mwakanolo amesema lengo ni kuona wahitaji wanasherekea sikuu ya Eid El Fitri kama jamii nyingine.

"Nimesimama kwa niaba ya Mkurugenzi wa nimekabidhi mchele kilo 400 na tende boksi 20 kikubwa ni kuona wenzetu wanasherekea kwa furaha kama jamii nyingine” amesema.

Wednesday, April 3, 2024

TULIA TRUST YATOA MSAAADA WA CHAKULA, MAVAZI KWA WAZEE WASIOJIWEZA

Wazee wasiojiweza Jijini Mbeya wameanza kutabasamu baada ya  Taasisi ya Tulia Trust kuanza program  ya kugawa chakula na mavazi  bure.

Programu hiyo imeanza leo katika baadhi ya Kata lengo ni kuhakikisha wahitaji wanafikiwa huku kikosi kazi cha Taasisi ya Tulia Trust kikiendesha zoezi hilo kulingana na idadi ya waliobainika.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi hiyo, Joshua Mwakanolo amesema lengo ni kuhakikisha wazee wasiojiweza wanatabasamu kwa kupata mahitaji muhimu.

Tuesday, April 2, 2024

MADAKTARI BINGWA KUWEKA KAMBI YA SIKU NNE HOSPITALI YA RUFAA KANDA MBEYA

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya (MZRH) kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya wameandaa kambi ya kutoa huduma upasuaji kwa watu wenye magonjwa mbalimbali.

Kambi hiyo itahudumiwa kwa ushirikiano wa madaktari bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambao ni wataalamu wa magonjwa ya ubongo, mishipa ya fahamu, saratani pamoja na magonjwa ya mifupa.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji amesema kambi hiyo itachukua siku nne kuanzia Aprili 8 hadi Aprili 12, 2024 na baada ya muda huo kuisha huduma hizo zitaendelea kutolewa katika hospitali hiyo.

Monday, April 1, 2024

MWALIMU NA MWANAFUNZI WAUAWA CHUNYA

Na Ezekiel Kamanga.

Watu wawili wakazi wa Kiwanja Kata ya Mbugani Wilayani Chunya, Mkoani Mbeya wanadaiwa kuuawa na mtoto mwingine mwenye umri wa miaka sita kujeruhiwa kwa vitu vyenye ncha kali nyumbani kwao.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa aliyeuawa ni mwalimu Herieth Lupembe wa shule ya msingi Mbugani aliyefahamika kwa jina la Herieth Lupembe mwingine ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza sekondari ya lsenyela aliyekuwa anaishi naye.

Taarifa za mauaji hayo zilipatikana jioni machi 30, 2024 baada ya mwalimu huyo kutofungua duka lake na simu yake kutopatikana pia kutoonekana kanisani wakati si kawaida yake.

Baadhi ya mashuda wamedai kuwa aliagiza bidhaa za dukani kutoka Mbeya baada ya kutoonekana bidhaa hizo ziliachwa nje.

Taarifa zilitolewa kijijini kwa mwenyekiti Gideon Kinyamagiha ambapo uongozi ulitoa taarifa Polisi ambao nao walifika na kufanya uchunguzi wa awali kisha kuchukua miili na kwenda kuihifadhi Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa uchunguzi zaidi ambapo majeruhi amekimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.

Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga kuthibitisha chanzo cha tukio hilo la kinyama.