Friday, November 29, 2024

WENYEVITI WAONYWA KUTOKUWA CHANZO CHA MIGOGORO

Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Mohamed Fakii ameonya wenyeviti wa serikali za mitaa kuepuka kuwa chanzo cha migogoro na badala yake kuimarisha ulinzi shirikishi na usalama wa raia na mali zao.
 
Mohamed amesema leo Novemba 28, 2024 wakati akiwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa kwenye tukio la kuapishwa wenyeviti 181 na wajumbe 908 katika mitaa, vitongoji na kata.
 
Amesema wenyeviti baada ya kuapishwe wakawe chachu kwa wananchi na sio kugeuka wababe wakati wa kuwatumikia makujumu yako kwenye maeneo yao ya kazi.

Monday, November 25, 2024

BENKI YA PBZ YAUNGA MKONO UMOJA WA BAJAJI NA BODABODA

Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) imetoa pikipiki 10 zikiwepo za matairi matatu (bajaji) mbili kwa  umoja wa bajaji na bodaboda jiji la Mbeya kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali kuwezesha vijana kujiajiri

Meneja Masoko na Uendelezaji wa Benki ya PBZ Mohamed Ismail amesema jana Novemba 25, 2024 mara baada ya kumkabidhi Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackon kwenye maadhimisho ya miaka 15 ya umoja wa bajaji Jiji la Mbeya yaliyo fanyika viwanja vya Mwenge.

Ismail amesema kwa kutambua vijana ni chachu ya maendeleo na namna gani Mbunge wetu na Spika Dkt. Tulia Ackson anavyowekeza kusaidia vijana kujiajiri.

DKT. TULIA, TFS WAZINDUA KAMPENI UPANDAJI MITI MILIONI MBILI

Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Dkt. Tulia Ackson amehamasisha jamii kugeukia matumizi ya nishati safi na kutunza mazingira kwa kupanda miti rafiki.

Dkt. Tulia ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) amesema jana Jumatatu Novemba 25, 2024 wakati uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji upandaji miti iliyohusisha Wakala wa Huduma za Misitu (TFS).

Amesema katika kampeni hiyo wanatarajia kupanda miti  milioni mbili ya kivuli yenye uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Kampeni hiyo imehusisha upandaji miti katika Taasisi za Serikali zikiwepo Shule za Msingi na Sekondari Mkoa wa Mbeya na kugusa kata 36.

JESHI LA POLISI MBEYA LATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI

Kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 nchini, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendesha mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari mkoani humo kuhusu masuala ya uchaguzi.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Novemba 23, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania Tawi la Mbeya, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amesema kuwa Jeshi la Polisi lipo imara kuhakikisha linasimamia sheria, kanuni na taratibu wakati wa uchaguzi na halitasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayebainika kukiuka.

Kamanda Kuzaga amewataka Waandishi wa Habari kuwa wazalendo na kutumia taaluma yao kuwajulisha wananchi mchakato mzima wa uchaguzi jinsi unavyoenda na kutoa elimu kuhusu haki na wajibu wa mpiga kura.

DKT. TULIA ACKSON ASHIRIKI IBADA MADHABAHU YA SAUTI YA UPONYAJI NA REHEMA ISYESYE JIJINI MBEYA

Rais wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson ameshiriki ibada Kanisa la Baptist Isyesye Madhabahu ya Sauti ya Rehema na sauti ya uponyajiKata ya Isyesye huduma inayoongozwa na Mchungaji Patrick Mwalusamba ambapo amewahimiza Waumini kuendelea kuombea amani nchini huku akiwasisitiza kushiki uchaguzi utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.

Dkt. Tulia Ackson amesema Waumini wanawajibu wa kwenda kusikiliza kampeni za uchaguzi ili wapate viongozi watakaowaletea maendeleo katika mitaa yao. Pia ameipongeza huduma hiyo kwa namna inavyozidi kukua siku hadi siku.

Dkt. Tulia Ackson amesema Waumini wasiposhiriki kupiga kura wasiwe na sababu za kuwalaumu viongozi watakaochaguliwa kwa kuwa wao wameshindwa kuitumia fursa hiyo.

UTPC KUZINDUA KAMPENI YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA NOVEMBA 25, MKOANI MANYARA

Kuelekea Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) umejipanga kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kupitia mtandao wa WhatsApp, pamoja na mitandao mwingine ya kijamii kwa kushirikiana na klabu 28 zilizopo mikoa yote ya Tanzania . Kampeni hii itazinduliwa rasmi Novemba 25 Mkoani Manyara.

Friday, November 22, 2024

CHAUMA KUFANYA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KIDIGITALI

Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) Mkoa wa Mbeya Ipyana Njiku amesema chama hiyo kimeamua kufanya kampeni kidigitali kwa kupita mitaani na kipaza sauti ili kutokuleta usumbufu kwa wananchi wakati wakiendelea na shughuli zao.

WAPINZANI WASHINDWA KUSIMAMISHA WAGOMBEA KWENYE MITAA 53 MBARALI

Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mkoa wa Mbeya Bahati Ndingo amesema wamejipanga CCM kushinda kwa  kishindo katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa Novemba 27, 2024 na kuwataka wananchi kuendelea kukiamini.

Ndingo amesema jana Novemba 21, 2024 wakati wa uzinduzi wa kampeni za kuelekea uchaguzi mdogo zilizo fanyika katika kata ya Ubaruku huku mgeni rasmi akiwa aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa.

"Tuna uhakika Mbarali kushinda kwa kura za kishindo uchaguzi wa serikali za mitaa wagomea tulio wasimamisha tuna imani nao kwa asilimia 100 na kwamba mitaa 53 watapita bila kupingwa baada ya upinzani kutosimamisha wagombea" amesema Ndingo.

Wednesday, November 20, 2024

MSD MAKAO MAKUU WATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA KUJIONE HUDUMA ZINAZOTOLEWA

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya leo Novemba 20, 2024 imetembelewa Ujumbe maalumu kutoka Bohari ya Dawa (MSD) ulioambatana na mjumbe wa bodi, uongozi wa juu wa bohari ya Dawa kutoka makao makuu pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Kanda ya Nyanda za juu kusini.

Lengo la ujumbe huo kutembelea hospitalini hapa ni kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa kupitia ushirikiano uliopo pamoja na kujadiliana mambo mbalimbali kwa lengo la kuboresha maeneo mbalimbali ya utoaji huduma kupitia mapungufu yanayojitokeza ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

 

Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na kuwekaza jitihada mbalimbali katika ubunifu kupitia wataalamu wa ndani ili kupunguza gharama mbalimbali zinazoweza kujitokeza hasa katika swala la uboreshaji na ukarabati wa vifaa tiba pindi vinapopata hitirafu.

Thursday, November 14, 2024

WAMUOMBA MBUNGE KUKAMILIKA JENGO KITUO SHIKIZI


Wananchi wa kijiji cha Mpolo Wilaya Mbarali Mkoa wa Mbeya wameomba Mbunge wa Jimbo hilo, Bahati Ndingo kuwasaidia kukamilisha jengo la kituo cha elimu shikizi ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi.

Ombi hill wamelitoa jana Novemba 14, 2024 kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mbunge huyo uliolenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Mkazi wa kijiji cha Mpola Shija Masanja amesema ukosefu wa shule shikizi umepelekea watoto kutembea umbali mrefu kufuata elimu.

Wakati huo huo wameomba kuboreshwa miundombinu ya barabara, umeme kijijini hapo ili kuwasaidia kuchochea shughuli za kiuchumi.

TDB KUHAMASISHA PROGRAMU YA UNYWAJI WA MAZIWA KUKABILIANA NA UDUMAVU

Serikali kwa kushirikiana na Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) imekuja na programu ya uhamasishaji unywaji maziwa ikilenga kuwafikia wanafunzi 100,000 katika shule 140 nchini.

Programu hiyo imefika katika mikoa nane ukiwepo Mkoa wa Mbeya sambamba na kutengeneza fursa ya usambazaji kwa wasindikaji wadogo kufikisha huduma mashuleni.

Kaimu Meneja wa Bodi ya Maziwa, Joseph Semu amesema jana Novemba 14, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ujio wa programu hiyo kwa Mkoa wa Mbeya.

Monday, November 11, 2024

DKT. TULIA AWASHUKIA WANAO TELEKEZA WAZAZI KWA IMANI POTOFU

Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson amekemea tabia ya baadhi ya familia kuwa na utamaduni wa kutelekeza wazazi kwa kutanguliza imani za kishirikina.

Dkt. Tulia ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mbunge Duniani (IPU) amesema jana Novemba 11, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa mtaa wa Inyara Kata ya Iyunga.

Kauli ameitoa wakati akikabidhi nyumba kwa wajane Tusekile Lumbalile (88) na Mwaine Lumbalile (86) ambao ni ndugu wa familia moja wanaoishi bila msaada wa familia.

"Ndugu zangu inaumiza sana hawa wakina mama walipaswa watunzwe na familia zao lakini wanaishi peke yao huku changamoto ni kujengeka na kuamini imani potofu za kishirikina" amesema.

Tuesday, November 5, 2024

CHINA YAINGIA MAKUBALIANO NA TAASISI YA TULIA TRUST KUKUZA UTAMADUNI

Taasisi ya Tulia Trust imeingia makubaliano na kikundi cha ngoma za asili cha Wu Opera kupitia kituo cha Zhejiang Wu Opera Research Centre Of China kwa lengo la kukuza utamaduni baina ya nchi hizo mbili.

Taasisi hiyo ambayo Mkurugenzi wake Spika wa Bunge Mbunge wa Mbeya mjini na Rais wa Umoja wa Mabunge Dunuani (IPU) Dkt. Tulia Ackson imeingia makubaliano hayo leo Novemba 4, 2024.



Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust Joshua Mwakanolo amesema lengo ni kukuza utamaduni na asili baina ya nchi ya Tanzania na China kubadilishana tamaduni zetu, lugha na mtindo.