Saturday, January 13, 2024

MRADI WA TACTICS WA BILIONI 85 KUGUSA MASOKO YA SOWETO NA SOKOMATOLA, JIJINI MBEYA.

Halmashauri ya Jiji la Mbeya iko mbioni kusaini mkataba wa ujenzi wa Soko la Soweto na Sokomatola kupitia mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) kwa ufadhiri wa Benki ya Dunia.

Akizungumza na Mwandishi wa habari leo Jumamosi, Januari 13, 2024 Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Dourmohamed Issa amesema tayari wameanza zabuni ya tenda kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya masoko hayo.

“Soko la Sokomatola na Soweto yanakwenda kujegwa kisasa zaidi na kutengeza taswira nzuri kwa Jiji la Mbeya na kabla ya mradi kuanza kuna maeneo yametengwa kwa ajili ya kuwahamishia wafanyabishara wanaopisha mradi huo” amesema Issa.


Issa amesema mbali na mradi huo wa TACTIC Jiji limeweka mipango ya kuboresha miundombinu ya baadhi ya masoko kupitia mapato ya ndani lengo ni kuhakikisha Wafanyabishara wadogo wanakuwa salama.

Mstahiki Meya ameongeza kuwa mbali na kuanza ujenzi wa masoko katika awamu ya kwanza tayari kuna miundombunu ya barabara za pembezoni nimejengwa sambamba na mtaro maji kutoka Kata ya Nzovwe mpaka Iyela wenye urefu wa kilometa 6.45 .

Issa ametaja barabara zilizojengwa kupitia mradi wa TACTIC kwa ufadhiri wa benki ya dunia ni pamoja na Iziwa kilometa (2.5)  Kalobe (3.5) Ilomba kwenda Machinjioni mpaka Mapelele, Uyole kwenda Itezi (3.8)  Kabwe - Block T mpaka SIDO (1.2) hali ambayo imesaidia kurahisisha shughuli za kiuchumi .

Kwa upande wake Diwani Kata ya Maendeleo Issa Shaban amesema ujio wa mradi huo utaongeza chachu ya upatikanaji wa huduma kwa jamii hususan kupunguza adha kwenye Soko la sasa .

Amesema katika kutekeleza mradi huo zaidi ya wafanyabishara 486 wataondolewa na kuhamishiwa eneo la kiwanja ngoma ambako vitajengwa vizimba kwa ajili ya kuendesha biashara za kila siku.

No comments:

Post a Comment