Monday, January 22, 2024

DKT. TULIA AKABIDHI MAHITAJI KWA WANAFUNZI 3,000 WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU, JIJINI MBEYA.


Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Spika wa Bunge na Mbunge Mbeya mjini, Dkt. Tulia Ackson ametoa msaada wa mahitaji zikiwepo sare za shule kwa wanafunzi 3,000 wanaotoka mazingira magumu.

Dkt. Tulia amekabidhi mahitahi hayo katika viwanja vya Stendi ya Mabasi Kabwe leo Jumatatu Januari 22, 2024 huku akikumbusha jamii kusaidia kundi hilo kupata elimu kama jamii nyingine.

“Kuna watu uwa wanajiuliza kwanini ninaposaidia watu lazima wapigwe picha,ni lazima kufanya hivyo lengo ni kuikumbusha jamii kusaidia wahitaji katika maeneo tunayotoka” amesema.


Dkt. Tulia amesema kuwa sio misaada hiyo  ameguswa kuona hakuna mtoto ambaye atashindwa kuhudhuria masomo kwa kukosa mahitaji ikiwepo sare za shule, dafrari na mengineyo.
“Tunaona Rais Samia Suluhu Hassan amewekeza kwenye elimu nami kama Mama ni lazima niguse kundi hili ili kujenga kizazi ambacho kitakuja kuwa tegemeo kwa taifa la sasa na kizazi kijacho” amesema.
Wakati huo huo amesema kuwa Serikali itaendelea kuboresha sekta ya elimu sambamba na kuwataka  watanzania kuwa na utamaduni wa kusaidia watoto wanaoishi mazingira magumu.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Dourmohamed Issa amesema uwepo wa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kumejenga heshima kwa Jiji la Mbeya kwa ushirikiano hakuna changamoto za miundombinu ya vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo na madawati.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amesema wanalodeni kubwa kwani Dkt. Tulia amekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya elimu, afya na kufanya majukumu ambayo yalikuwa yatekelezwe na Serikali.

Kwa upande wake Chifu wa Jiji la Mbeya, Rocket Mwanshinga amekemea tabia ya baadhi ya wananchi kumbeza na kwamba huo ni wivu.
 
“Dk Tulia umetupa heshima kuwa wanambeya tutakulinda kwani tangu uchaguliwe kuwa Mbunge tunaona Mbeya ya kisasa tofauti na miaka ya nyuma” amesema.


No comments:

Post a Comment