Sunday, January 28, 2024

MZRH YAWAKARIBISHA MADAKTARI BINGWA NA WAUGUZI WALIOKUA MASOMONI.

 

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya jana Januari 27, 2024 imefanya hafla fupi ya iliyoandaliwa kwaajili ya kuwakaribisha madaktari bingwa na wauguzi ambao walikuwa masomoni.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika bustani ya Mbeya Peak, madaktari bingwa walipewa fursa ya kuzungumza na kuelezea uzoefu wao katika masomo yao na jinsi walivyopata maarifa na ujuzi mpya. Walishirikisha pia changamoto walizokutana nazo na jinsi walivyoweza kuzishinda.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, Dkt. Godlove Mbwanji, aliwapongeza na kuwashukuru madaktari na wauguzi waliokuwa masomoni. Pia, alielezea furaha yake kuona sehemu kubwa ya wafanyakazi waliotoka masomoni ni wanafunzi bora "best students" katika vyuo vyao.

Hafla hiyo ilikuwa fursa nzuri ya kuimarisha ushirikiano na kuchochea maendeleo ya hospitali. Madaktari na wauguzi hao walitambuliwa kama wataalamu wenye ujuzi mkubwa ambao watachangia katika kuboresha huduma kwa wagonjwa wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.





No comments:

Post a Comment