Tuesday, January 23, 2024

CHAKULA CHA MCHANA KWA WANAFUNZI KINAVYOLETA TIJA KATIKA UFUNDISHAJI

Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa kushirikiana na wazazi imeendelea na Mpango wake kuhakikisha kila Mwanafunzi anapata chakula cha mchana kwa siku zote za masomo.

 
Uongozi wa shule ya Msingi Masebe na Mpuguso zilizopo Ushirika (Kata ya Mpuguso) zinatekeleza mpango huu. Shule ya Msingi Masebe imenufaika na ujenzi wa Uzio wa shule kupitia Wakala wa barabara Mjini na Vijijini (TARURA) ikiwa ni sehemu ya Marejesho (Corporate Social Responsibility) baada ya wananchi kutoa ushirikiano katika ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Lami umbali wa KM 7.5 kutoka Masebe - Lutete.
 
Chakula cha Mchana kinatolewa kwa wanafunzi wote katika Wilaya ya Rungwe. Hatua ya utoaji chakula shuleni umeongeza ufaulu katika shule mbalimbali. Mathalani katika mtihani wa taifa (NECTA) Mwaka uliopita ufaulu umefikia 96.5% kwa darasa la nne na 94.4% kwa darasa la Saba.
 
Hii imechangiwa na upatikanaji wa chakula cha mchana shuleni, kuzingatia weledi katika ufundishaji, uboreshaji wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia na serikali kuboresha stahiki za watumishi.

Aidha katika shule nyingi utoro umepungua kutokana na wanafunzi kupata chakula shuleni, pamoja na kushiriki michezo mbalimbali .

No comments:

Post a Comment