Sunday, January 28, 2024

MZRH YAWAKARIBISHA MADAKTARI BINGWA NA WAUGUZI WALIOKUA MASOMONI.

 

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya jana Januari 27, 2024 imefanya hafla fupi ya iliyoandaliwa kwaajili ya kuwakaribisha madaktari bingwa na wauguzi ambao walikuwa masomoni.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika bustani ya Mbeya Peak, madaktari bingwa walipewa fursa ya kuzungumza na kuelezea uzoefu wao katika masomo yao na jinsi walivyopata maarifa na ujuzi mpya. Walishirikisha pia changamoto walizokutana nazo na jinsi walivyoweza kuzishinda.

Saturday, January 27, 2024

MASHINDANO YA MBEYA TULIA MARATHON KUTIMUA VUMBI MEI 10 NA 11 SOKOINE, JIJINI MBEYA.

Mratibu wa Mashindano ya Mbeya Tulia Marathon, Lwiza John akionyesha sehemu ya  medali zitakazolewa kwa washindi wa mbio hizo zitakazofanyika Mei 10 na 11 mwaka huu.

Mashindano ya mbio za riadha maarufu kama  Mbeya Tulia Marathon yanatarajia kuanza kutimua vumbi katika viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya Mei 10 mpaka 11 mwaka huu.

Mashindano hayo yameandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust ambayo Mkurugenzi wake ni Rais wa Mabunge Duniani (IPU) ambae pia ni Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi hiyo, Joshua Mwakanolo amesema mashindano hayo yatahusisha mbio fupi na ndefu.

Tuesday, January 23, 2024

KT. TULIA AKABIDHI NYUMBA KWA MZEE MWENYE UHITAJI NONDE, JIJINI MBEYA.

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson amemkabidhi nyumba ya kuishi, kitanda na godoro Mzee Aswile Mwakigege mkazi wa Kata ya Nonde Jijini Mbeya.

Nyumba hiyo imekabidhiwa  leo Jumanne Januari 23,2024 katika hafla fupi  huku ikielezwa nyumba hiyo imejengwa kupitia taasisi yake ya Tulia Trust  ambayo Dkt Tulia ni Mkurugenzi.

Hatua ya Taasisi hiyo kumjengea nyumba ,mara Mzee Aswile ni baada ya makazi aliyokuwa akiishi kubomoka na kupelekea mzee huyo kukosa makazi rasmi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi nyumba hiyo, Dkt Tulia ameitaka jamii kuwakumbuka wazee wasiojiweza pale panapokuwa na mahitaji.

CHAKULA CHA MCHANA KWA WANAFUNZI KINAVYOLETA TIJA KATIKA UFUNDISHAJI

Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa kushirikiana na wazazi imeendelea na Mpango wake kuhakikisha kila Mwanafunzi anapata chakula cha mchana kwa siku zote za masomo.

 
Uongozi wa shule ya Msingi Masebe na Mpuguso zilizopo Ushirika (Kata ya Mpuguso) zinatekeleza mpango huu. Shule ya Msingi Masebe imenufaika na ujenzi wa Uzio wa shule kupitia Wakala wa barabara Mjini na Vijijini (TARURA) ikiwa ni sehemu ya Marejesho (Corporate Social Responsibility) baada ya wananchi kutoa ushirikiano katika ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Lami umbali wa KM 7.5 kutoka Masebe - Lutete.
 
Chakula cha Mchana kinatolewa kwa wanafunzi wote katika Wilaya ya Rungwe. Hatua ya utoaji chakula shuleni umeongeza ufaulu katika shule mbalimbali. Mathalani katika mtihani wa taifa (NECTA) Mwaka uliopita ufaulu umefikia 96.5% kwa darasa la nne na 94.4% kwa darasa la Saba.
 
Hii imechangiwa na upatikanaji wa chakula cha mchana shuleni, kuzingatia weledi katika ufundishaji, uboreshaji wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia na serikali kuboresha stahiki za watumishi.

Aidha katika shule nyingi utoro umepungua kutokana na wanafunzi kupata chakula shuleni, pamoja na kushiriki michezo mbalimbali .

Monday, January 22, 2024

DKT. TULIA AKABIDHI MAHITAJI KWA WANAFUNZI 3,000 WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU, JIJINI MBEYA.


Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Spika wa Bunge na Mbunge Mbeya mjini, Dkt. Tulia Ackson ametoa msaada wa mahitaji zikiwepo sare za shule kwa wanafunzi 3,000 wanaotoka mazingira magumu.

Dkt. Tulia amekabidhi mahitahi hayo katika viwanja vya Stendi ya Mabasi Kabwe leo Jumatatu Januari 22, 2024 huku akikumbusha jamii kusaidia kundi hilo kupata elimu kama jamii nyingine.

“Kuna watu uwa wanajiuliza kwanini ninaposaidia watu lazima wapigwe picha,ni lazima kufanya hivyo lengo ni kuikumbusha jamii kusaidia wahitaji katika maeneo tunayotoka” amesema.


Dkt. Tulia amesema kuwa sio misaada hiyo  ameguswa kuona hakuna mtoto ambaye atashindwa kuhudhuria masomo kwa kukosa mahitaji ikiwepo sare za shule, dafrari na mengineyo.
“Tunaona Rais Samia Suluhu Hassan amewekeza kwenye elimu nami kama Mama ni lazima niguse kundi hili ili kujenga kizazi ambacho kitakuja kuwa tegemeo kwa taifa la sasa na kizazi kijacho” amesema.

Sunday, January 21, 2024

WAZIRI JAFFO APIGA MARUFUKU UCHIMBAJI WA DHAHABU NDANI YA MTO ZIRA WILAYANI CHUNYA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akitoa maelekezo kwa watendaji wa mmoja wa migodi alitotembelea Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.

Sehemu ya bwawa linalotumika kutililisha tope lenye maji yenye kemikali ikiwa ni utekelezaji wa takwa kisheria.

Serikali imepiga marufuku shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu na kuchenjua katika Mto Zira Kata ya Ifumbo Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya mpaka wataalam watakapofika kufanya tathimini ya mazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na  Mazingira Seleman Jaffo, amesema hayo juzi wilayani Chunya wakati akiwa kwenye ziara ya kutembelea Kampuni ya G&I ambayo ilisitishiwa uzalishaji katika mto huo.

Jaffo amesema katika ziara yake miongoni mwa maeneo yaliyo msukuma ni kujiridhisha  shughuli za uchimbaji zinazofanywa kwenye mto huo, sambamba na kutoa mwelekeo wa Wizara kutoruhusu shughuli hizo mpaka wataalam watakapofanya tathimini.

MASACHE AKABIDHI GARI LA WAGONJWA HOSPTALI YA WILAYA CHUNYA.


Mbunge wa Jimbo la Lupa Masache Kasaka amekabidhi gari la Wagonjwa kwa uongozi wa Hosptali ya Wilaya ya Chunya ambayo ilipandishwa hadhi kutoka kituo cha afya.

Masache amesema gari hilo la wagonjwa (Ambulance) limetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika vituo vya Kambikatoto na Lupa Wilayani humo.

Amesema Serikali itaendelea kuboresha sekta ya afya ambapo imetoa zaidi ya Sh 2.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa majengo nane sambamba na Sh 400 milioni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba.

“Kama inavyofahamika hosptali hii awali ilikuwa kituo cha afya, Serikali ikapandisha hadhi na kuwa Kituo cha Afya, miundombinu yake ilikuwa sio rafiki lakini kwa kipindi cha miaka miwili tunashuhudia miundombinu imeboreshwa  chini ya Serikali ya awamu ya sita” amesema Masache.

Masache pia amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali sambamba na kuwataka kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mdogo wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika hivi karibuni.

“Sitarajii kuona kuna watu wengine watachukua fomu kuwania nafasi hiyo kwani hawa waliopo wanatosha wameonyesha uwezo mkubwa kushiriki katika usimamizi wa miradi ya Maendeleo iliyoelekezwa na Serikali” amesema Masache.

Saturday, January 13, 2024

MRADI WA TACTICS WA BILIONI 85 KUGUSA MASOKO YA SOWETO NA SOKOMATOLA, JIJINI MBEYA.

Halmashauri ya Jiji la Mbeya iko mbioni kusaini mkataba wa ujenzi wa Soko la Soweto na Sokomatola kupitia mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) kwa ufadhiri wa Benki ya Dunia.

Akizungumza na Mwandishi wa habari leo Jumamosi, Januari 13, 2024 Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Dourmohamed Issa amesema tayari wameanza zabuni ya tenda kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya masoko hayo.

“Soko la Sokomatola na Soweto yanakwenda kujegwa kisasa zaidi na kutengeza taswira nzuri kwa Jiji la Mbeya na kabla ya mradi kuanza kuna maeneo yametengwa kwa ajili ya kuwahamishia wafanyabishara wanaopisha mradi huo” amesema Issa.

Wednesday, January 10, 2024

WANAUME KUTOSHIRIKI KLINIKI KUNACHANGIA KUTOTENGWA BAJETI ZA LISHE KATIKA FAMILIA

Wadau wakiwemo wazazi wakiwa katika kituo maalumu cha Malezi Jumuishi kilichofunguliwa na Taasisi ya WeCare Foundation kwaajili ya kutoa elimu ya afua za malezi stahiki kwa watoto ikiwemo lishe bora katika Hospitali ya Agakhan tawi la Mbeya. (Picha na Joachim Nyambo)

 

Hatua ya wanaume kutohudhuria kliniki wakati wenza wao wakiwa wajawazito au wanapokuwa wamejifungua inatajwa kuwa chanzo cha familia nyingi kutotenga bajeti ya milo sahihi kwa wanawake wajawazito, wanaonyonyesha na pia watoto wanaotimiza umri wa miezi sita tangu kuzaliwa.

 

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa Makala haya umebaini kuwa licha ya wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi binafsi na za serikali kutilia mkazo suala la uhamasishaji wanaume kuhudhuria kliniki pamoja na wenza wao bado mwamko ni mdogo.

 

Wadau wakiwemo wauguzi waliozungumzia hali hiyo wanasema ni wanaume wachache ambao wanaona umuhimu wa kwenda na wenza wao kliniki wanapokuwa wajawazito au wanapowapeleka watoto wachanga.