Mbunge wa Jimbo la Mbeya vijiji Oran Njeza ameishauri serikali kuondoa makusanyo ya kodi za majengo kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenda serikali za mitaa.
Njeza amesema Bunge limeshauri kuhakikisha kiwango cha asilimia 20 ya mapato ya kodi za majengo zielekezwe kwenye Halmashauri kwa wakati.
Mbunge huyo ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha bungeni taarifa ya kamati ya bunge kwa mwaka wa fedha 2024.
Amesema katika mwaka fedha 2024/2025 serikali iongeze kiwango kinacho rejeshwa katika halmashauri kutoka asilimia 20 mpaka 50 ili kuharakisha zoezi la uthamishaji wa majengo na kurejesha asilimia 20.
Sambamba na hilo Mbunge Njeza amesema bunge limeshauri kuboreshwe mfumo wa tausi katika ukusanyaji wa mapato ya majengo sambamba na kuongeza idadi ya wataalamu ili kurahisisha utekelezaji.
Taarifa hiyo imeungwa mkono na wananchi huku wakieleza itawezesha kulipa kwa hiyari kodi ya majengo tofauti na makusanyo kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA).
Thursday, February 13, 2025
NJEZA: BUNGE LIMESHAURI UKUSANYAJI KODI ZA MAJENGO UREJESHWE SERIKALI ZA MITAA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment