Mdhamini mkuu wa mashindano hayo, mdau wa michezo nchini, Chief Godlove Mwakibete ambaye mbali na udhamini amechangia mahitaji mbalimbali na zawadi kwa washindi.
Akizungumza na waandishi wa habari, amesema ameguswa kudhamini lengo ni kuunga mkono juhudi za serikali kuhamasisha michezo na kuibua vipaji vya vijana mashuleni na kuviendeleza.
"Vijana tunahitaji kuunga mkono serikali kuwekeza katika michezo kwa kuibua vipaji vya wanafunzi na kuvikuza kupitia michuano mbalimbali kwa kutambua michezo nia afya, michezo ni fursa ya ajira" amesema Mwakibete.
Mbali na udhamini wa mashindano hayo, Chifu Godlove, amechangia mahitaji mbalimbali yakiwepo madawati 100, jezi kwa timu 120 zilizo shiriki, ng'ombe 6, na mbuzi wawili kwa ajili ya zawadi kama chachu ya kuongeza morari ya kufanya vizuri.
"Mimi ni mzaliwa wa Kyela nimeshiriki sana mashindano hayo nikiwa shule ya msingi sekondari miaka kadhaa iliyopita, nilipopata barua ya kuombwa udhamini sikusita, lakini pia sitaishia hapa nitaunga mkono jitihada mbalimbali katika jamii" amesema.
Ofisa michezo na utamaduni Wilaya ya Kyela, Zephania Jumbe amesema uwepo wa mshindano hayo ni chachu ya kuibua vipaji vitakavyo zalisha wa chezaji wakubwa.

No comments:
Post a Comment