Tuesday, February 4, 2025

DC MALISA AHIMIZA WANANCHI KUJENGA UTAMADUNI WA KUPIMA SARATANI

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya ili kukabiliana na ugonjwa saratani, huku takwimu zikionyesha watu 500 wamepatiwa huduma baada ya kubainika.

Malisa amesema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera kwenye Maadhimisho ya siku Saratani Duniani yaliyofanyika leo Jumanne Februari 4, 2024 katika Hosptali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH).

"Niwasisitize wananchi kupima afya mara kwa mara tunaona takwimu zinaonyesha watu 500 wamegundulika kuwa na saratani hususani kwa wanawake na wanaume" amesema Malisa.

Mkurugenzi mtendaji Hosptali ya Rufaa Kanda Dkt. Godlove Mbwanji amesema anaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuanza ujenzi wa huduma za mionzi ya saratani katika Mikoa saba ya Nyanda za Juu Kusini.

Amesena uwepo wa kituo hicho kitapunguza gharama kwa wagonjwa kusafiri kwenda Taasisi ya saratani ya Ocen Road Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mbwanji amesema saratani inatibika hivyo ni vyema wananchi kuwa na utaratibu wa kupima afya ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo uchangia vifo kwa kiwango kikubwa.

 Daktari Bingwa wa Saratani Hosptali ya Rufaa Kanda Dkt. Tibera Rugambwa amesema kati ya watu 45,000 wanaobainika na saratani  wastani wa watu 17,000 sawa na asilimia 37 ya watu upoteza maisha nchini.

Ametaja saratani inayoongoza kwa vifo kwa wanawake ni saratani ya mlango kizazi na matiti, huku kwa wanaume ni tezi dume na mfumo wa chakula.

Amesema kuwa changamoto kubwa ni hofu kwa wagonjwa baada ya kubainika sambamba na mira na desturi kwa kujenga imani saratani haitibiki.

Dkt. Tibera amesema kutokana na changamoto hiyo wanaendelea kutoa elimu kwa jamii kujitokeza kupima afya ili kujikinga mapema na magonjwa ya saratani.

No comments:

Post a Comment