Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson ameungana na Mama Lishe katika Kata ya Uyole Jijini Mbeya kwa ajili ya kuandaa chakula kwa kutumia nishati safi ya gesi.
Dkt. Tulia ameshiriki tukio hilo leo Jumatatu Septemba 30, 2024 kwa kuingia sokoni kufanya mahitaji mbalimbali huku akieleza lengo ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nishafi safi.
"Leo nashirikiana na Mama lishe kuandaa chakula kwa kutumia nishati safi lengo ni kuona wanabadilika kwa kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ili kulinda mazingira na kutunza rasilimali za miti" amesema Dkt. Tulia.
Dkt. Tulia ambaye ameambana na wadau wa kampuni ya nishati safi ya Oryx kwa ajili ya ugawaji wa majiko bure kwa mama lishe ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kutunza mazingira
Amesema lengo ni kuhamasisha jamii matumizi ya nishati ya gesi na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa.
"Mnaona hapa nimetumia muda mfupi kuandaa chakula lakini pia tunatunza mazingira yetu kwa jamii hususan mama lishe katika jiji la Mbeya" amesema.
Hata hivyo baadhi ya wananchi jijini Mbeya wamepongeza hatua ya Spika Dkt. Tulia ya kuingia jikoni kushirikiana na mama lishe hali ambayo itasaidia kushawishi wananchi kuachana na matumizi ya mkaa na kuni.
Kwa upande wake Peter Ndomba Meneja miradi kampuni ya Oryx amesema mpaka sasa wamewafikia wajasirimali zaidi ya 70, nchini huku lengo ni kuwafikia wengi zaidi.
Amesema mbali na Dkt. Tulia kushiriki mapishi pia watagawa mitungi ya gesi kwa mama lishe zaidi ya 30 lengo ni kuhamasisha matumizi nishati sasa ya kupikia.
No comments:
Post a Comment