Wednesday, September 25, 2024

DC MALISA: WANANCHI WASHIRIKI KUPINGA UKATILI

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amehamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika kampani ya "Tuwalinde kabla hawaja haribikiwa" kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto mashuleni.

Malisa amesema leo mara baada ya kuzindua kampeni hiyo huku akisisitiza wazazi, walezi na jamii kutekeleza majukumu yao kuwalinda watoto ili kuwa katika mazingira salama.

"Wazazi, walezi tekelezeni majukumu yenu kulinda na kuwa karibu na watoto ili kubaini changamoto zinazowakabili na kuwasilisha katika vyombo vya dola" amesema.


DC Malisa amesema lengo la serikali kuja na kampeni hiyo kulinda watoto na kukabiliana na matukio ya mmonyoko wa maadili miongoni mwa jamii na kwamba  haitasita kuwashughulikia watu watakao jihusisha na vitendo vya ukatili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema awali kampeni hiyo ilizinduliwa katika Mkoa wa Njombe yenye lengo la kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ubakaji na vipigo.

Mkuu wa Dawati la Jinsia Jeshi la Polisi Mkoa Veronica Ponela amesema awali wamebaini watoto na vijana wengi hawajua athari za matukio ya ukatili ujio wa kampeni hiyo utakuwa suruhisho na mwarobaini wa matukio ya ukatili.

Amesema kampeni hiyo itafanyika mashuleni,vyuo vya kati sambamba na shule za msingi na sekondari lengo ni kuondoa watoto katika dhana ya kuathirika na vitendo hivyo.


No comments:

Post a Comment