Monday, June 30, 2025

MASACHE ACHUKUA FOMU YA KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA UBUNGE WA JIMBO LA LUPA, CHUNYA

Mbunge wa Jimbo la Lupa Masache Kasaka amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya ubunge wa Jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM leo Juni 30, 2025.


 

MWALUNENGE AREJESHA FOMU YA KUOMBA RIDHAA YA KUGOMBEA UBUNGE MBEYA MJINI

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge amerejesha fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Mbeya Mjini leo Juni 30, 2025.



 

Sunday, June 29, 2025

MHANDISI MARYPRISCA MAHUNDI ACHUKUA FOMU KUTETEA NAFASI YAKE

Mhandisi Maryprisca Mahundi amefika katika ofisi za UWT Mkoa wa Mbeya kuchukua fomu ya kugombea Ubunge Viti Maalum Mkoa wa Mbeya.

Mhandisi Maryprisca Mahundi amechukua fomu hiyo ili kutetea nafasi yake ambayo ameitumikia muhula mmoja wa miaka mitano (2020-2025).

 

MWANAHABARI AJITOSA KUMKABILI MEYA WA JIJI LA MBEYA

Mwandishi wa Habari, David Nyembe (kushoto), akikabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Isanga kuchaguliwa kuwa mgombea udiwani wa Kata hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu.

Nyembe amekabidhiwa fomu na Katibu wa CCM Kata hiyo Golden Ndolela leo Juni 29, 2025.


Hadi kufikia leo majira ya saa nne asubuhi jumla ya wagombea watatu tayari wamechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho kuwania nafasi hiyo akiwemo aliyekuwa Meya wa Jiji la Mbeya Mh. Dormohamed Issa.

 

Friday, June 20, 2025

HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA MATIBABU YA MACHO KWA WATOTO

 

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH) imepatiwa msaada wa vifaa tiba, vifaa saidizi na mashine ya kisasa ya Ultra Sound kwaajili ya kutoela matibabu ya macho wa watoto wanaofikishwa hospitali kwaajili ya matibabu, venye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100, kutoka kwa Shirika la Kilimanjaro Center for Community Ophthalmology (KCCO) kama sehemu ya juhudi za kuboresha huduma za matibabu ya macho kwa watoto wa nyanda za juu kusini mwa Tanzania.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Martin Mutayoba, Mwakilishi wa Shirika la KCOO Nyanda za Juu Kusini, amesema kuwa shirika hilo limekuwa likifanya kazi kwa karibu na hospitali (MZRH) kwa huduma za matibabu ya macho pia kupitia huduma mkoba za matibabu ya macho kwa watoto kwa ufanisi zaidi.

Ameongeza kuwa msaada huo ni matokeo ya ushirikiano wanaopatiwa hivyo amewataka watumiaji wa vifaa hivyo kuvihifadhi vizuri ili viendelee kufanya kazi kwa ubora.

Wednesday, June 18, 2025

NJEZA ATEMBELEA WAFIWA AJALI ILIYOUA 29 MLIMA IWAMBI

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini  Oran M. Njeza, amezitembele na kutoa mkono wa pole kwa familia za watu 29 waliofariki na majeruhi  wa ajali.

Ajali hiyo ilitokea  Juni 7, 2025 katika mtelemko mkali wa mlima Iwambi Wilaya ya Mbeya, baada ya ya lori lilokuwa limebeba shehena za unga kugonga  magari mawili yakiwepo ya abiria.

Katika ajali hiyo watu 28 walipoteza maisha papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa na kukimbizwa katika Hosptali Teule ya Ifisi Wilaya ya Mbeya.


Wednesday, June 11, 2025

DC MALISA AMKABIDHI MEYA JIJI LA MBEYA KITABU MPANGO MKAKATI MIAKA MITANO

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Malisa amezindua mpango mkakati wa Dira ya miaka mitano ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya na kumkabidhi rasmi Meya Jiji la Mbeya Dour Mohamed  Issa

Makabidhiano hayo yamefanyika leo Jumatano Juni 11, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa  mkapa jijini hapa, ikiwa ni uzinduzi wa mpango mkakati wa dira ya miaka mitano ya 2025/26 mpaka 2029/2039 kwa halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Dira hiyo imebeba vipaumbele 29 ikiwepo masuala ya elimu, afya  maboresho ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ujenzi wa bandari ya nchi kavu, sekta ya afya na elimu na mengineyo mengi.


Malisa amepongeza wadau walio fanikisha Halmashauri ya Jiji kutekeleza  mkakati, huku akitaka kuweka kipaumbele katika uboreshwaji miundombunu ya masoko ili wafanya biashara waweze kufanya kazi masaa 24.