Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson ameungana na Mama Lishe katika Kata ya Uyole Jijini Mbeya kwa ajili ya kuandaa chakula kwa kutumia nishati safi ya gesi.
Dkt. Tulia ameshiriki tukio hilo leo Jumatatu Septemba 30, 2024 kwa kuingia sokoni kufanya mahitaji mbalimbali huku akieleza lengo ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nishafi safi.
"Leo nashirikiana na Mama lishe kuandaa chakula kwa kutumia nishati safi lengo ni kuona wanabadilika kwa kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ili kulinda mazingira na kutunza rasilimali za miti" amesema Dkt. Tulia.