WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Jumatano,
Januari 20, 2021 amekagua kitalu cha miche ya mkonge cha TARI Mlingano
kilichopo wilayani Muheza, Tanga na kufungua zoezi la ugawaji wa miche
kwa wakulima wa zao hilo.
Akizungumza wakati wa tukio hilo Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zinazolima mkonge nchini pamoja na wakulima wakubwa wa mkonge watenge ekari 10 kwa ajili ya kuanzisha vitalu vya kuzalisha miche ya mkonge ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa miche ya mkonge

Amesema kituo cha TARI Mlingano
kinatakiwa kijikite katika kufanya utafiti wa mbegu bora pamoja na
dawa za kudhibiti magonjwa katika zao hilo na suala la uzalishaji wa
mbegu lifanywe kwa ushirikiano katika ya kituo hicho na wadau wa zao
hilo.
Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Kilimo itenge fedha katika bajeti yake kwa ajili ya kituo cha TARI Mlingano ili kukiwezesha kupanua eneo la uzalishaji miche kwa kununua vitendea kazi yakiwemo matrekta.
No comments:
Post a Comment