Friday, December 27, 2024

MWEF YATOA MSAADA KWA HOSPITALI YA WAZAZI META

Taasisi ya Maryprisca Women Impowerment Foundation (MWEF) inayoongozwa na Naibu Waziri wa  Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi imetembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa ajili ya kutoa msaada kwa wazazi waliojifungua siku ya sikukuu ya Christmas.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Maryprisca Women Impowerment Foundation Adam Simbaya amesema lengo la kutembea Hospitali ya wazazi Meta ni kumshukuru Mungu pia akianisha zawadi zilizotolewa kuwa ni pamoja na maziwa, sabuni, pampas na wipes.

Aidha Simbaya amesema wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye amekuwa akiyagusa makundi mbalimbali yakiwemo ya wanawake na watoto.

Sunday, December 15, 2024

JAJI MWAMBEGELE "KUJIANDIKISHA KUWA MPIGA KURA ZAIDI YA MARA MOJA NI KOSA LA JINAI"

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini imewaasa wananchi kujiepusha na kosa la kujiandisha zaidi ya mara moja kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kutakiwa kujiandikisha mara moja na kwenye kituo kimoja ili kuepuka uvunjaji wa sheria.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Jacob Mwambegele katika Mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura umefanyika Jijini Mbeya leo Disemba 15, 2024.

"Kujiandikisha kuwa mpiga kura zaidi ya mara moja ni kosa la jinai, 'mtu yeyote atakaeomba kuandikishwa zaidi ya mara moja atakuwa ametenda kosa la jinai na akitiwa hatiani adhabu yake ni faini isiyopungua kiasi cha shilingi laki moja na isiyozidi laki tatu au kutumikia kifungo kisichopungua miezi sita na kisichozidi miaka miwili gerezani au vyote kwa pamoja" amesema Jaji Mwambegele.

Thursday, December 12, 2024

DKT. TULIA APOKEA MASHINE YA UPASUAJI NA KITANDA KWA WAJAWAZITO

Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson, amekabidhiwa mashine ya upasuaji na kitanda cha kisasa kwa ajili ya wajawazito vyenye thamani ya Sh Milioni 102 .

Vifaa hivyo vimetolewa kwa kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya vilovyotolewa na wadau wa Maendeleo.

Dkt. Tulia amepokea vifaa hivyo kutoka kwa mwakilishi wa wadau hao Noelah Msuya jana Desemba 12, 2024 na kisha kukabidhi kwa uongozi wa Hosptali ya Rufaa ya Mkoa.

Dkt,Tulia ameipongeza Serikali kwa jitihada zake endelevu katika kuboresha sekta ya afya ikiwemo kujenga vituo vya  afya ili kuwasogezea wananchi wake huduma ya karibu.

WAKULIMA WATAKIWA KULIPA MADENI MSIMU 2023/24

Chama cha Msingi cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku (Lualaje Amcos) kimewataka wakulima kulipa madeni kwa wakati ili kuepuka kupigwa mnada kwa mali zao ikiwepo mashamba .

Mwenyekiti wa Lualaje Amcos, Alberto Kacheza amesema leo Desemba 12, 2024 kwenye mkutano mkuu 41 wa mwaka wa kupitia taarifa mapato na matumizi hali ya uzalishaji kwa msimu huu wa kilimo.

Kacheza amesema kuna baadhi ya wakulima kwa makusudi wamekuwa wakilimbikiza madeni ya mikopo ya pembeo kwa makusudi hali inayopelekea kupata hati za mashaka

"Leo tumepitia taarifa mbalimbali sambamba na mwenendo Amcos yetu na kupendeleza masuala ya msimu wa kilimo 2024/25 katika uwekezaji wenye tija kwenye kilimo cha tumbaku na hatua za kuwachukulia wakulima wasiorejesha fedha za mikopo" amesema.

Friday, December 6, 2024

MHANDISI MARYPRISCA MAHUNDI ACHANGIA MIL. 3.4 NA TOFALI KIKUNDI CHA GWALUGANO ISANGE

Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ameunga mkono juhudi za Kikundi cha UWT Gwalugano Isange chenye mtaji wa shilingi milioni tisini huku akikichangia shilingi milioni tatu na laki nne pia tofali elfu moja za saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mradi.

Katika hotuba yake Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka wanawake kupendana na kuwataka waendelee kuwahamasisha wengine kujiunga ili kila mwanamke amiliki uchumi wake ambapo amewataka wanawake kuchangamkia mikopo inayotolewa na Halmashauri.

Mbali ya kukipongeza kikundi hicho amesema changamoto wazichukulie kama fursa akikazia kampeni yake ya wanawake na uchumi pia akiwahimiza kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan.