Tuesday, July 29, 2025

Saturday, July 26, 2025

MWAKIPESILE AMPONGEZA DKT. SAMIA KWA KUENDESHA MKUTANO KIDIGITALI

AJALI YAUA WANAFUNZI WATANO WAKIKIMBIA MCHAKAMCHAKA, CHUNYA MBEYA


Wanafunzi watano wa Sekondari ya Chalangwa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wamefariki kwa kugongwa na basi lenye namba za usajili namba T 194 DCE aina ya YUTONG linalomilikwa na Kampuni ya Safina linalofanya safari zake Lualaje Mbeya Julai 26, 2025 majira ya saa 11:30 alfajiri barabara kuu ya Chunya Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Wilbert Siwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo wanafunzi watano wamefariki papo hapo na majeruhi tisa wamepokelewa Kituo cha Afya Chalangwa.

Siwa amesema mara baada ya tukio dereva wa basi hilo alitoroka na juhudi za kumtafuta zinaendelea ambapo ametoa wito kwa madereva kuwa waangalifu wawapo barabarani na chanzo kikitajwa ni mwendo kasi na uzembe wa dereva.

Thursday, July 17, 2025

TULIA TRUST YAREJESHA TABASAMU FAMILIA NYUMBA ILIYOTEKETEA MOTO


Taasisi ya Tulia Trust inayojihusisha na uwekezaji  kiuchumi wananchi imeanza ukarabati wa nyumba ya familia ya Mzee Ayoub Wakazi wa Kata ya Nsalaga Jijijini hapa.

Nyumba hiyo iliteketea kutokana na janga la moto lililotokea hivi karibuni hali iliyosababisha kukosa mahala pa kuishi.


Ukarabati huo unatekelezwa na Taasisi ya Tulia Trust  ambayo Mkurugenzi wake ni Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson na Rais wa Mabunge Duniani (IPU), kupitia mpango wa Tulia Trust mtaani kwetu.

Mpango huo umekuwa na tija ya kurejesha tabasamu kwa wananachi wa Jiji la Mbeya zikiwepo kaya zisizojiweza, yatima na wazee.

Thursday, July 10, 2025

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA MDUDE

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya imetupilia mbali maombi ya jinai namba 14538/2025 yaliyofunguliwa mei 17,2025 na Sije Mbughi mke wa Mpaluka Nyagali (Mdude) dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Mkurugenzi wa mashitaka (DPP), Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya(RPC), Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Mbeya (RCO) na askari Shaban Charo anayedaiwa kuwa ndiye aliyemchukua Mdude ambapo maombi yameanza kusikilizwa Juni 30, 2025 na kutolewa uamuzi Julai 9, 2025 na Jaji Said Kalunde.

Mleta maombi Sije Mbughi amewakilishwa na Wakili Bonifase Mwabukusi, Wakili Hekima Mwasipu na Wakili Solomon Kamunyu ambapo upande wa wajibu maombi umewakilishwa na Wakili Domick Mushi pamoja na Wakili Adalbert Zegge huku Sije akitaka mumewe kufikishwa mahakamani na kufungulia mashitaka kwa mujibu wa sheria.

Jaji Said Kalunde ameanza kutoa uamuzi majira ya saa 9:35 alasiri na kuhitimishwa saa 11:50 jioni awali Jaji Said Kalunde amesema upande wa mleta maombi akiwemo Sije Mbughi na Ezekiel Sheyo.