Wednesday, April 9, 2025

"TUPO TAYARI KWA UCHAGUZI, ILA TUNATAKA MABADILIKO HAYA" CHAUMMA

Pamoja na kuthibitisha kushiriki Uchaguzi Mkuu mwaka huu, Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimependekeza na kuishauri Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi baadhi ya mambo kufanyiwa marekebisho kabla ya zoezi hilo.

Tanzania inatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu, Oktoba 25 mwaka huu kuwapata madiwani, wabunge na Rais, huku Chama hicho kikitarajia kusimamisha wagombea katika nafasi zote.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa Aprili 7, 2025, Katibu Mwenezi wa Chama hicho Taifa, Ipyana Njiku amesema katika kikao cha Halmashauri kuu ya Chama hicho Februari 19, 2025 kiliazimia kushiriki uchaguzi huo katika nafasi zote na kutoa mwelekeo wa nchi kwa miaka mitano ijayo.