Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa, amehamasisha wananchi kutumia fursa ya ujio wa Madaktari Bingwa Bobezi wa Dkt Samia kufanyiwa vipimo vya uchunguzi wa magonjwa.
Kambi ya madaktari bingwa bobezi imeanza leo Mei 5 mpaka Mei 9, 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya (Mbeya RRH) kwa muda wa siku tano.
Amesema huduma hizo zitawanufaisha wananchi kutoka mikoa Nyanda za Juu Kusini ikiwepo Mbeya, Ruvuma Songwe, Songea Njombe.
Awali mkazi wa Njombe Vaileth Kwese,amesema kitendo cha serikali kuwafikishia huduma kimewapunguzia gharama za kusafiri umbali mrefu kufuata matibabu.